Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mzozo Sudan: Baraza la kijeshi lawakamata waliokuwa maafisa wa serikali





Raia Khartoum wameapa kuendelea na maandamano mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia

Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan limewakamata waliokuwa maafisa wa serikali na kuahidi kutowatawanya waandamanaji.

Msemaji mmoja pia ameuomba upinzani kumchagua waziri mkuu mpya na kuahidi kumuidhinisha watakayemchagua.

Maandamano ya miezi kadhaa nchni Sudan yamechangia kutimuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini Sudan Omar al-Bashir Alhamisi wiki iliyopita


Waandamanaji wameapa kusalia mitaani mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia

Raia wanaendelea kuandamana na wamekita kambi nje ya makao makuu ya wizara ya ulinzi katika mji mkuu Khartoum.

Je baraza la kijeshi limesema nini?

Katika mkutano na waandishi habari siku ya Jumapili, msemaji Meja Jenerali Shams Ad-din Shanto ameeleza kwamba baraza la kijeshi lipo "tayari kuidhinisha" serikali yoyote ya kiraia itakayoidhinishwa na vyama vya upinzani.

"Hatutomteua waziri mkuu. Watamchagua," alisema akimaanisha upinzani na makundi yanayoandamana.

Ameeleza pia kwamba jeshi halitowaondoa waaandamanaji kwa lazima lakini ametoa wito kwa waandamanaji hao "kuruhusu maisha yaendelee kama kawaida" na waache kuweka vizuzi kinyume cha sheria.

"Kushika silaha hakutoruhusiwa," aliongeza

Baraza la kijeshi pia limetangaza baadhi ya maamuzi yakiwemo:

Viongozi wapya wa jeshi na polisi


Mkuu mpya wa kitengo cha ujasusi (NISS)


Kamati za kupambana na rushwa na kuchunguza chama tawala kilichoondoka


Kuondolewa kwa marufuku zote na kubanwa kwa vyombo vya habari


Kuachiwa kwa maafisa wa polisi na jeshi waliozuiwa kwa kuungamkono waandamanaji.


Ukaguzi wa wajumbe wa kidiplomasia, na hatua ya kutimuliwa kwa balozi wa Sudan nchini marekani na Uswizi.



Kitu gani kimekuwa kilifanyika Sudan?

Maandamano ya kupinga kupanda gharama ya maisha yalianza Desemba mwaka jana lakini punde tu yakageuka kuwa wito mkubwa wa kumpinga rais bashir na utawala wake.

Siku ya Alhamisi Jeshi lilimtimua na kumzuia kiongozi huyo wa muda mrefu Sudan baada ya kuhudumu kwa miaka 30 madarakani.

Aliyeongoza mapinduzi hayo, waziri wa ulizni Awad Ibn Auf, alitangaza kwamba jeshi litasimamia serikali ya mpito kwa kipindi cha miaka miwili kitakachofuatwa kwa uchaguzi na akaidhinisha miezi mitatu ya hali ya dharura.


Lakini wandamanji waliapa kusalia mitaani hata baada ya hatua hiyo, wakitaka maguezi na kuidhinishwa kwa serikali ya kiraia mara moja.

Ibn Auf himself alijiuzuliu ziku ya pili , kama alivyojiuzulu mkuu wa usalama anayeogopwa na wengi Jenerali Salah Gosh.

Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan baada ya hapo alitajwa kuwa kiongozi wa baraza la mpito la kijeshi, kuwa kiongozi wa tatu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha siku nyingi.


Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan ndiye mkuu mpya wa baraza la mpito la kijeshi Sudan

Katika hotuba kwenye televisheni siku ya Jumamosi, Jenerali Burhan aliapa "kuung'oa utawala", na kuahidi kuheshimu haki za binaadamu, kusitisha marufuku ya kutotoka nje, kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuvunjilia mbali serikali zote za majimbo, kuwashtaki waliowaua waandamanaji na kukabiliana na rushwa.

Lakini muungano wa wataalamu Sudan (SPA), ambao umekuwa ukiongoza maandamano hayo umesema muitikio wa baraza hilo "haukudhihirisha matakwa yoyote ya raia" na ametaka maandamano yaendelee.


Miongoni mwa matakwa yao ni kutaka idara ya ulinzi ifanyiwe mageuzi, "viongozi wafisadi" wakamatwe na kuvunjiliwa mbali makundi ya sungusungu yaliohudumu chini ya rais wa zamani Bashir.

Kiongozi huyo wa zamani hajulikani yuko wpai, lakini viongozi wa mapinduzi hayo wanasem ayumpo mahali salama.

Bashir ameshtakiwa kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binaadamu huko Darfur na mahakama ya kimatiafa ya jinai ICC

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.