Kard.Re:Roho Mtakatifu aangazie makardinali kupata Papa anayehitajika kwa wakati wetu

Kardinali Re (@Vatican Media) Katika misa kabla ya uchaguzi wa Papa mpya iliyoongozwa na Kadinali Re,Dekano wa Makardinali katika Kanisa Kuu la Vatican ameainisha kazi za kila mrithi wa Petro,kwa kuzingatia amri mpya ya upendo.Wito kwa makardinali wapiga kura:kuchagua kwa majukumu ya juu zaidi ya kibinadamu na ya kikanisa,kuepuka mawazo ya kibinafsi na kuangalia kwa manufaa ya Kanisa na ubinadamu. Na Angella Rwezaula – Vatican. Nitamwinua kuhani mwaminifu, atakayetenda sawasawa na haja za moyo wa Mungu ndiyo ilikuwa antifoni ya wimbo wa ufunguzi iliyosindikiza maandamano marefu ambayo asubuhi ya leo tarehe 7 Mei 2025 iliwaona wakiingia makardinali wateule kwa upole kama kawaida katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican lililojaa waamini elfu tano, wakati wa Misa ya Pro eligendo Romano Pontifice, yaani kabla ya kuchagua Papa wa Roma. Aliyeongoza misa hiyo katika madhabahu ya kukiri ni Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali. Katika mahali pa ...