KATIBA YA CCM YARUHUSU MIKUTANO YAKE KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, kufanya mabadiliko madogo ya Katiba ya CCM ambapo sasa Katiba hiyo inatambua ufanywaji wa mikutano ya ngazi mbalimbali kwa njia ya mtandao maarufu kama E- Meeting. Kulingana na Dkt. Samia wakati akitangaza mapendekezo hayo kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mabadiliko hayo ni katika kuhakikisha kuwa Chama hicho kinaenda sawa na mabadiliko mbalimbali ya teknolojia yanayotokea duniani,suala ambalo limewezesha CCM pia kufunga Mitambo ya teknolojia yenye kuwezesha Ngazi za CCM wilaya na Mikoa kuweza kuunganishwa pamoja na Makao Makuu kwa njia ya mtandao. Rais Samia amebainisha kuwa Idara ya Oganaizesheni ilipendekeza vikao vitakavyoweza kufanyika kimtandao ni Vikao vya Sekretarieti ya Wilaya, Kamati za siasa za wilaya, Sekretarieti za Mikoa, Kamati za siasa za Mikoa, sekretarieti ya Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kamati ...