GAB0N:Jean Ping, ametaka watu wasishirikiane na Ali Bongo

MTEULE THE BEST

Rais Ali Bongo (kushoto) Jean Ping (kulia)
Image copyrightGETTY IMAGES
Kiongozi wa upinzani Gabon, Jean Ping, ametaka watu wasishirikiane na Ali Bongo kama kiongozi wa taifa baada ya uchaguzi wa Agosti uliokumbwa na mzozo.
Kiongozi aliyepo sasa Bongo, alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo, lakini Ping anasisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda.
Upinzani unasema watu kadhaa waliuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi.
Jean PingImage copyrightAFP
Image captionJean Ping
Jean Ping ametia saini taarifa yake kama 'rais mteule' - wadhifa usiotambuliwa, na tume ya uchaguzi nchini.
Kiongozi huyo wa upinzani ameshutumu alichokitaja kuwa mapinduzi ya kijeshi katika uchaguzi dhidi yake.
Anataka raia wote wa Gabon wanaompinga rais Ali Bongo wajumuike na kushirikiana katika kumtenga kimataifa.
Bwana Ping ametaka pia Bongo aidhinishiwe vikwazo na viongozi wengine kadhaa akiwemo mkuu wa mahakama ya katiba iliyopinga malalmiko aliyowasilisha kupinga uchaguzi huo.
Lakini hatakama kuna wasiwasi wa kimataifa kuhusu uchaguzi huo, Rais Bongo haonekani kuwachia madaraka wakati wowote hivi karibuni.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU