Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionChristian Eriksen
Paris St-Germain wanaandaa pauni milioni 100 kwa ofa ya mchezaji wa Tottenham mwenye miaka 26 raia wa Denmark Christian Eriksen. (Express)
Schalke wana nia ya kumasaini mchezaji mwenye miaka 22 raia wa England Reuben Loftus-Cheek kwa mkopo lakini Chelsea haunda wasiruhusu kuondoka kwake. (Telegraph)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMatteo Darmian
Beki wa Manchester United Matteo Darmian anataka kuondoka Old Trafford na Juventus, Napoli na Internazionale wanamwinda mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Italia. (Manchester Evening News)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho aliachanganyikiwa kufuatia madai ya Paul Pogba ya kuwepo uhusiano mbaya kati yao siku ya Ijumaa. (Telegraph)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMarcus Bettinelli
Kipa Marcus Bettinelli, 26, anaweza akaamua kuondoka Fulham baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya kwanza ya msimu. (Mail)
Liverpool watasikiliza ofa kwa mchezaji wa maiaka 32 mlinzi rauia wa Estonia Ragnar Klavan. (Liverpool Echo)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionLee Cattermole
Kiungo wa kati wa Sunderland mwenye miaka 30 Lee Cattermole huenda akahamia Bordeaux, ambapo aliyekuwa meneja wa zamani wa Black Cats sasa ndiye meneja. (Teamtalk)
Wale wanaolengwa kuchukua nafasi ya mkurugenzi mpya wa Manchester United ni pamoja na kipa Edwin van der Sar, mkurugenzi wa Juventus Fabio Paratici na Monchi, mkurugenzi wa zamaniawa Sevilla na sasa Roma. (Independent)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWilfried Zaha
Mshambuliaji Wilfried Zaha anasema bado anazungumza na Crystal Palace kuhusu kuongezwa mkataba wake huko Selhurst Park. (Mail)
Meneja wa zamani wa Argentina Jorge Sampaoli anataka kurudi kwenye usimamizi na Mexico. (Goal)
Paris St-Germain na Monaco wanataka kiungo wa kati wa Sevilla mwenye miaka 29 Mfaransa Steven Nzonzi. (France Football)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMaxim Choupo-Moting
Kiungo wa kati mwenye miaka 25 Giannelli Imbula, kiungo wa kati mwenye miaka 32 msikochi Charlie Adam, winga raia wa Cameroon mwenye miaka 29 Maxim Choupo-Moting na mlinzi mwenye miaka 33 Geoff Cameron wote wana mpango wa kuondoka Stoke. (Telegraph)
Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui anataka kuongeza mlinzi na mshambuliaji kwenye kikosi chake kabla ya tarehe ya mwisho. (AS)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionJulen Lopetegui a
Bora zaidi kutoka Jumatatu
AC Milan wanamtafuta kiungo wa kati wa Chelsea mwenye miaka 23 Tiemoue Bakayoko kwa mkopo wa msimu wote kabla ya kumpa mkataba wa kudumu. (Sun)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionTiemoue Bakayoko
Barcelona itamwinda Paul Pogba baada ya msimu wa joto wa kununua wachezaji kukamilika tarehe 31 Agosti kufuatia kukubali kuwa Manchester United hawatamuuaza mchezaji huyo mwenye miaka 25 raia wa Ufarasa mwezi huu. (Telegraph)
Kipa wa Liverpool Loris Karius, 25, anawindwa na Besiktas. Klabu hiyo wa Uturuki imekuwa na mpango wa kumsaini Mjerumani huyo kwa mkopo wa msimu wote. (Sun)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionLoris Karius
Beki wa Manchester City mwenye miaka 23 Jason Denayer amekataa kuondoka kwa mkopo kwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji anataka kuhamia klabu ya Uturuki ya Galatasaray. (Star)
Cristiano Ronaldo amewashauri Juventus kumuendea kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Serbia amehusishwa na Manchester United na Chelsea. (Star)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionCristiano Ronaldo
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrina Rabiot, 23, amekataa ofa ya kusaini upya mkataka wake na mabingwa hao wa Ligue 1. Mkataba wa kwanza wa Mfaransa huyo unakamilika mwisho wa msimu. (L'Equipe
SHERIA 17 ZA SOKA ======================= Mchezo wa soka ni moja ya michezo maarufu sana duniani na ni biashara kubwa sana katika ulimwengu wa michezo na ukitaka kuamini hili angalia makampuni yaliyowekeza katika kudhamini soka – ni makampuni makubwa makubwa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa. Kwa kuzingatia aina hii ya wadhamini, waendeshaji wa mchezo wa soka, wameweka kanuni na miongozo ya kufuatwa ili kuhakikisha kuwa wale wanaowekeza pesa zao wanaona thamani ya uwekezaji wao. Kwa hiyo soka kama ilivyo katika michezo mingine inazo kanuni na tutajadili kanuni moja baada ya nyingine kama zilivobainishwa katika muongozo wa FIFA unaojulikana kwa jina la Law of the Game. Sheria Namba 1: Dimba ============== NYASI - Dimba la soka litakuwa la nyasi asilia au bandia kulingana na kanuni za masindano na nyasi hizo lazima ziwe za rangi ya kijani. Kwa dimba la nyasi bandia na kama mchezo unaochezwa utakuwa wa kutambuliwa na FIFA, basi nyasi hizo bandia lazima zikidhi viwango maalumu ...
Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi. Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria. Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao. Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...
MTEULE THE BEST TUMSIFU YESU KRISTO WAPENDWA KATIKA BWANA!!! MADA YA LEO: KUMTUMAINIA MUNGU SOMO; zaburi 11:1-7 Kwake MWENYEZI-MUNGU nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia "ruka kama ndege mpaka mlimani" Maana waovu wanavuta pinde wameweka mishale tayari juu ya uta wawapige mshale watu wema gizani! Kama misingi ikiaribiwa mtu mwadilifu atafanya nini? MWENYEZI-MUNGU yumo hekaluni mwake takatifu ; kiti cha enzi cha MWENYEZI-MUNGU kiko mbinguni Kwa macho yake huwachungulia wanadamu na kujua kila kitu wanachofanya MWENYEZI-MUNGU hupima waadilifu na waovu huwachukia kabisa watu wakatili Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberti upepo wa hari ndiyo itakuwa adhabu yao MWENYEZI-MUNGU ni mwadilifu na apenda uadilifu watu wanyoofu watakaa pamoja naye NENO LA BWANA Unaruhusiwa kuchangia funguka tupate maoni yako MUNGU AKUBARIKI
Maoni