Papa Francis amelazwa katika hospitali ya Gemelli kutokana na matatizo ya kupumua.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis (86), amelazwa katika hospitali ya Gemelli kutokana na matatizo ya kupumua.

Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema kuwa katika siku za karibuni Kiongozi huyo amekuwa akilalamika kuhusu shida hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki imeeleza matokeo ya vipimo kuwa ni tatizo kwenye mfumo wa upumuaji. Aidha Vatican imesisitiza kuwa Papa Francis hana Uviko19.

Awali Vatican ilieleza kuwa Kiongozi huyo alipelekwa hospital ili kufanyiwa ukaguzi ambao ulishapangwa.

Hata hivyo vyombo vya habari vya Italia vilihoji suala hilo kwani mahojiano ya televisheni aliyotakiwa kufanya Papa jioni ya leo yalifutwa dakika za mwisho.

Maoni

Unknown alisema…
MUNGU AMBARIKI NA AMPONYE KWA NJIA YESU KRISTO BWANA WETU AMINA
Unknown alisema…
MUNGU AMBARIKI NA AMPONYE KWA NJIA YESU KRISTO BWANA WETU

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU