MAREKANI YAHIMIZA AMANI DRC 23

Marekani yahimiza amani DRC huku mkataba wa usitisha mapigano kati ya serikali na M23 ukiafikiwa

hatua hii ni ishara ya hatua iliyopigwa baada ya mazungumzo yaliyochukuwa miezi kadhaa iliyoandaliwa nchini Qatar

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kundi la waasi la M23, wamekubaliana kutia saini azimio la kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa DRC.

Kwa mujibu wa waangalizi wa mzozo huo, hatua hii ni ishara ya hatua iliyopigwa baada ya mazungumzo yaliyochukuwa miezi kadhaa iliyoandaliwa nchini Qatar, japo taarifa za ziada kuhusu walichokizungumzia na kukubaliana hazijawekwa wazi.

Azimio hilo linalotarajiwa kutiwa saini Jumamosi hii jijini Doha, linatangazwa wakati ambapo Marekani imezidisha shinikizo lake kwa pande husika kukamilisha masuala muhimu kwenye majadiliano hayo yanayotarajiwa kurejesha amani katika eneo la Mashariki mwa Congo.

Hatua hii huenda ikavutia wawekezaji kutoka wa mataifa ya Magharibi ambao wanatarajiwa kuwekeza mabilioni ya dola za Marekani kwenye eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini kama vile tantalum, dhahabu,cobalt, shaba nyekundu, lithium miongoni mwa mengine mengi.

Kundi la M23, lililoyateka maeneo ya mashariki mwa nchi limekuwal ikikabiliana na jeshi la FARDC mashariki mwa DRC, hatua yao kubwa ya hivi maajuzi ilikuwa kuteka na kudhibiti mji wa Goma, mwezi Januari na baada ya hapo limepiga hatua kubwa ya kudhibiti na kukalia eneo kubwa katika majimbo mawili ya Kivu Kusini na Kivu Kasakazini.

Vita hivyo vimesababisha maafa ya maelfu ya watu na kuwalazimu mamilioni zaidi kukimbia makwao kwa ajili ya usalama wao.

Makabiliano hayo kwa wakati mmoja yalitishia kuzua vita vikuu katika eneo hilo, na kusambaa hadi katika ukanda mzima na kuyahusisha mataifa jirani. Mataifa Jirani yametuma majeshi yao kwenye eneo hilo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU