Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Muuaji wa Jo Cox ajigamba mahakamani

MTEULE THE BEST   Muuaji wa Jo Cox ajigamba mahakamani   Thomas Mair, mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mbunge wa Uingereza amefikishwa mahakamani Central London. Alipoambiwa aseme jina lake, mtu huyo mwenye umri wa miaka hamsini na mbili alisema nikimnukuu ''jina langu ni kifo kwa wasaliti,uhuru kwa Uingereza''. Mair pia ameshtakiwa kwa kumdhuru vibaya Cox,kupatikana na bunduki na silaha nyingine hatari.   Marehemu Jo Cox Marehemu Cox aliyekuwa akiwakilisha chama cha upinzani cha leba alipigwa risasi na kudungwa kisu katika eneo lake la uakilishi siku ya alhamisi. Kifo chake kimesababisha kusitishwa kwa majuma kadhaa kampeini za kura ya maoini juu ya Uingereza kujiondoa katika uanachama wa muungano wa EU  

Auawa akiwa katika facebook

MTEULE THE BEST     Auawa akiwa katika facebook live-stream     mtu mmoja nchini Chicago alipigwa risasi akiwa katika video ya moja kwa moja inayojulikana kama Live_stream katika mtandao wa Facebook ,polisi wamesema. Antonio Perkins mwenye umri wa miaka 28 alipigwa risasi katika kichwa na shingo magharibi mwa mji huo. Kanda hiyo ya video bado iko katika facebook na imeangaliwa mara 700,000. Ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu mjini Chicago ambapo mauaji yamefanyika moja kwa moja katika mtandao wa facebook. Mnamo mwezi Machi mtu asiyejulikana alipigwa risasi mara 16 wakati akipeperusha matangazo hewani. Hakuna mtu aliyekamatwa kufika sasa.Programu ya live-streaming ya facebook inawaruhusu watu kutangaza moja kwa moja mtandaoni .  

Auawa akichuma kuvu yenye 'nguvu za kiume'

MTEULE THE BEST       Mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika kijiji cha Nepal alipokuwa akichuma kuvu fulani inayotambuliwa kwa uwezo wake wa kuongeza nguvu za kiume. Kuvu hiyo inayotambulika kama ''Himalayan Viagra'' inasemekana kuwaongezea ashki walaji wake. Kuvu hiyo ni kitega uchumi cha wenye vijiji wa maeneo ya milimani. Haijulikani kwanini genge hilo la wavamizi liliwashambulia watu hao waliokuwa wakichuma kuvu hiyo katika wilaya ya mugu ila maafisa wa utawala wamethibitisha kuwa watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulizi hilo. Ukungu au kuvu hiyo humea kwenye mwili wa nondo au mtoto wa kipepeo na kilo moja ya kuvu hiyo inaweza kuuza kwa maelfu ya dola za Marekani nchini Uchina.   Auawa akichuma kuvu yenye 'nguvu za kiume' ...

Mohammed Morsi ahukumiwa kifungo cha maisha

MTEULE THE BEST     Mohammed Morsi ahukumiwa kifungo cha maisha     Mahakama ya Misri imempatia kifungo cha maisha jela aliyekuwa rais wa Kiislamu Mohammed Morsi baada ya kukamilika kwa kesi yake ya upelelezi. Ni miongoni mwa washtakiwa wanaoshtumiwa kwa kutoa nakala za siri kwa taifa la Qatar. Wakili wa Bw Morsi amesema kuwa aliwachiliwa huru kwa upelelezi lakini akapewa hukumu hiyo kutokana na kuliongoza kundi haramu. Wengine ni waandishi wawili wa Aljazeera ambao walihukumiwa kifo wakiwa hawako mahakamani.                             Aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi Hatahivyo kiongozi huyo wa zamani ana uwe...

KUMTUMAINIA MUNGU

MTEULE THE BEST TUMSIFU YESU KRISTO WAPENDWA KATIKA BWANA!!! MADA YA LEO: KUMTUMAINIA MUNGU SOMO; zaburi 11:1-7   Kwake MWENYEZI-MUNGU nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia "ruka kama ndege mpaka mlimani" Maana waovu wanavuta pinde wameweka mishale  tayari juu ya uta wawapige mshale watu wema gizani! Kama misingi ikiaribiwa mtu mwadilifu atafanya nini? MWENYEZI-MUNGU yumo hekaluni mwake takatifu ; kiti cha enzi cha MWENYEZI-MUNGU kiko mbinguni  Kwa macho yake huwachungulia wanadamu  na kujua kila  kitu wanachofanya MWENYEZI-MUNGU hupima waadilifu na waovu  huwachukia kabisa  watu wakatili  Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberti upepo wa hari ndiyo itakuwa adhabu yao  MWENYEZI-MUNGU ni mwadilifu na apenda uadilifu watu wanyoofu watakaa pamoja naye NENO LA BWANA Unaruhusiwa kuchangia funguka tupate maoni yako MUNGU AKUBARIKI  

Picha za utupu hupunguza hamu ya kufanya mapenzi

MTEULE THE BEST   Picha za utupu hupunguza hamu ya kufanya mapenzi Watoto wengi hupata njia ya kutazama picha za ngono mitandaoni wakiwa na umri mdogo, kwa mujibu wa utafiti. Karibu asilimia 53 ya watoto walio kati ya umri wa miaka 11 na 16 wametizama picha za ngono mitandaoni, wote wakiwa ni asilimia 94, ya walioona picha hizo wakiwa na umri wa miaka 14 kulingana na utafiti wa chuo cha Middlesex. Utafiti huo unasema kuwa vijana kama hao, wako kwenye hatari ya kupoteza hamu ya kushiriki mapenzi. Serikali inasema kuwa ili kuhakikisha kuwa watoto wako salama na masuala ya mitandao ni jukumu kubwa. Watafiti waliwahoji watoto 1,001 walio na umri kati ya miaka 11 na 16, na kugundua kuwa asilimia 65 ya wale walio na umri wa kati ya miaka 15-16, walikubali kuona picha za ngono sawa na asilimia 28 ya wale walio kati ya miaka 11 na 12.  

TANZANIA KUFANYA BIASHARA NA QATAR

MTEULE THE BEST   Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa taifa lake linakusudia kufanya biashara na jamhuri ya Qatar haswa katika sekta ya gesi na usafiri wa ndege. Rais Magufuli aliyasema hayo baada ya kukutana na balozi wa Qatar nchini Tanzania bwana Abdallah Jassim Al Maadadi. Aidha rais Magufuli alitangaza nia ya kufungua ubalozi wa Tanzania mjini Doha kwa lengo la ''kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na taifa hilo tajiri la ghuba. "Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" amesema bw Magufuli. TZ yataka uzoefu wa Qatar sekta ya gesi Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na mkurugenzi wa mawa...