Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Duke suruali kuto oa

MTEULE THE BEST Spika wa bunge katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kano, amesema kwa umma utaombwa kutoa maoni yake kuhusu mswada wenye lengo la kuwazuia wanaume maskini kuoa zaidi ya mke mmoja. Alhassan Rurum aliiambia BBC kuwa viongozi na wasomi wataombwa ushauri kuhusu ni tata t haswa atatambuliwa kuwa maskini. Sheria ya kuzuia wanaume kuoa wake wengi kutangazwa Nigeria Waliokamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa waachiliwa Pendekezo hilo lenye utata lilitolewa na Muhammad Sanusi II, ambaye ni Emir wa Kano, kuhakisha kuwa wanaume wana familia ambazo wanaweza kuzitunza.

MAARAMIA SOMALIA WATEKA MELI

MTEULE THE BEST Taarifa kutoka Somalia zinasema maharamia wa Kisomali wameiteka meli ya mizigo ya India. Kumezuka utata kuhusu eneo halisi ambako meli hiyo ya kutoka India ilikotekwa. Baadhi ya vyombo vya habari nchini vinaarifu kuwa tukio hilo linaarifiwa kutokea Somalia ya kati, eneo la Elhur kiasi ya kilomita 50 kusini mwa Hobyo, eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa ndio kitovu cha maharamia wa Kisomali. Kaimu rais wa eneo la Galmud, Somalia ya kati ameithibitishia BBC kwamba meli ya mizigo imetekwa siku ya Jumamosi karibu na eneo la Haradhere. Ameeleza kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea Kismayo. Wakati huo huo maafisa huko Puntland wanasema utekaji huo umefanyika katika eneo lao. Inaarifiwa kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea Yemen kutoka India wakati ilipotekwa na ina mabaharia 11 ndani. Mapema mwezi uliopta maharamia katika eneo la Puntland waliiteka meli ya mafuta ambayo baadaye waliachia huru. Kilikuwa ni kisa cha kwanza cha uharamia kushuhudiwa tan...

BARUA KWA MH.RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO TANZANIA

MTEULE THE BEST Kwako Mheshimiwa Rais, Kwanza kabisa nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuongoza taifa hili la Tanzania na pia pole kwa majukumu uliyonayo,kuna mengi mazuri unayafanya huenda sisi watanzania wa kawaida hatuyaelewi na kuona unakosea ila naamini mwisho wa siku tutaelewa. Lengo la ujumbe huu kwako ni kuhusiana na kilio tulichonacho sisi vijana ambao kwa muda sasa tunasubiri ajira. Ni muda wa miezi 9 umepita tangu uliposema mbele ya vyombo vya habari kuwa zoezi la uhakiki litadumu mwezi mmoja na nusu haitozidi miwili utakuwa umetoa ajira ambapo wengi tukawa tuna matumaini kuwa zitatoka ajira zile 71,000 lakini mpaka leo kwa taarifa mzitoazo ni kuwa mmetoa ajira 5000 kuachia mbali za wakurugenzi na wenyeviti wa taasisi mbalimbali. Si kweli kwamba vijana wote ni wavivu na tumeshindwa kujiongeza la hasha kinachopelekea tuonekane wazembe, hatuwezi kujiongeza,mizigo kwa wazazi,hatutaki kujiajiri sababu kubwa ni hizo ahadi zenu mnazotupa za miezi miwili miwili...

Korea kusini kutoa pesa KWA watu wanaoikimbia Korea kaskazin

MTEULE THE BEST Korea kusini imeidhinisha nyongeza ya fedha inazotoa kama malipo kwa watu wanaoasi uraia wao kutoka nchi jirani ya Korea Kaskazini,kwa lengo la kupata habari muhimu za kujasusi. Hatua hiyo pia ina walenga wanajeshi wanaovuka mpaka wakiwa na zana za kijeshi. Waasi waliyo na taarifa muhimu itakayo saidia kuimarisha usalama wa Korea Kusini, watapokea,fedha ya hadi dola 860,000 Wizara ya masuala ya muungano imesema, sheria hiyo mpya, itaongeza ruzuku ya vifaa vitakavyo ingizwa nchini humo na waasi hao. Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia atimuliwa Polisi nchini Malaysia wagundua kilichomuua Kim Jong Nam Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong-nam alilipwa $90 Vifaa hivyo ni kama vile meli na karakana ya kijeshi. Hii ni mara ya kwanza kwa nyongeza kama hiyo kutolewa katika kipindi cha miaka ishirini. Lengo la hatua hiyo ni wazi kuwa, Korea Kusini inataka kuongeza idadi ya watu wanaobadilisha uraia wa Korea kaskazini kujiunga nayo. Serikali ya Korea Kaskazi...

Rais Magufuli ameweka nadhiri yake

MTEULE THE BEST RAIS MAGUFULI SIO WA MCHEZO KILA KUKICHA TANZANIA YAKE INAPIGA HATUA MBELE , RAIS MAGUFULI  RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania John Magufuli, ameweka mikakati imara.Hayumbishwi kwa kile anachokiiamini kuwa anafanya kwhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kiuchumi ambayo anaitekeleza kwa kasi kubwa    Moja ya mambo anayoyaamini kuwa yatasimamisha uchumi wa Tanzania nia pamoja na kujenga viwanda nchini.  Katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF umeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi Makubaliano haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa makao Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es Salaam. katika makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya kiwanda cha viatu cha karanga ambacho uzalish...

Tume za Haki za Binadamu kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Burundi zakutana

MTEULE THE BEST Tume za Haki za Binadamu kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Burundi zimekutana nchini Tanzania kujadili namna ambavyo tume hizo zinaweza kusimamia viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Utawala bora, amani na haki za binadamu. Akifungua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema mkutano huo utatoa tadhmni ya miaka 3 ya utendaji wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, sambamba na kutoa mapendekezo mapya kwa nchi hizo hasa katika kutatua migogoro na kulinda amani. Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Marry Massay amesema tume hizo zinawajibu wa kuhakikisha haki inazingatiwa, kutatua migogoro baina ya wananchi na viongozi wao na kushugulikia malalamiko. Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu kutoka nchini Burundi Jean Baribonekeza amesema hali ya Burundi kwa sasa imeimarika tofauti na mwaka mmoja ulipita ikiwa ni juhudi ya tum...