Maafisa nchini Kenya wamemkamata mkuu wa shirika la huduma kwa vijana NYS kama sehemu ya uchunguzi kuhusu kuibiwa kwa takriban dola milioni 100 katika shirika hilo. Vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la huduma kwa vijana NYS Richard Ndubai amekamatwa mapema leo pamoja na maafisa wengine wakiwemo mahasibu na maafisa wanaosimamia ununuzi wa vifaa NYS pamoja na wafanyabiashara waliohusika katika kandarasi na zabuni kadhaa. Mkuu wa idara ya upelelezi amesema watu 17 wamekamatwa ili kuhojiwa kuhusiana na kashfa hiyo ya ufisadi inayoikumba NYS. Mwendesha mkuu wa mashitaka pia amesema mashitaka dhidi ya washukiwa waliotajwa katika kashfa hiyo yataanza mara moja. Hata hivyo majina ya washukiwa hayajatolewa hadharani. Mabilioni yapotea NYS Vituo vya televisheni vya K24 na Citizen vimeripoti kuwa katibu wa kudumu wa wizara ya utumishi kwa umma, vijana na jinsia Lilian Mbogo Omollo amejisalilisha kwa polisi akiwa ameandamana na mawaki...