Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Taifa Stars ya Amunike usipime, yafufua matumaini ya Cameroon

MATUMAINI YA KUENDA  CAMEROON YAFUFUKA CHEREKO! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuichapa bila huruma Cape Verde kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa Afrika nchini Cameroon mwakani.  Stars inayonolewa na staa wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Nigeria, Emmanuel Amunike imepata ushindi huo kufuatia magoli yaliyofungwa kila kipindi na mastaa wake wanaocheza soka la kimataifa, Simon Msuva anaecheza Morocco akifunga goli la kwanza huku Nahodha Mbwana Samatta 'Poppa' akifunga goli la pili.  Samatta ambaye anakipiga Genk ya Ubelgiji inayoshiriki pia michuano ya Europa angeweza kuipa Stars goli baada ya mkwaju wake aliopiga kugonga mwamba kabla ya dakika chache mbele kutengeneza goli la kuongoza lililofungwa na Msuva

Serikali yagomea wapelelezi wa nje kuchunguza sakata la MO Dewji

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Serikali haiwezi kuruhusu vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nje ya nchi kuchunguza tukio la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.  Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 16, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari.  Amesema anaamini polisi kuna wataalamu wanaoijua kazi yao, wanaifanya kwa kuzingatia maadili.  “Kuna haja gani kuleta vyombo vya nje wakati tuna jeshi bora na lenye uelewa mkubwa licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale,” amesema.  Amesema  polisi hawajashindwa kuchunguza jambo hilo na lipo ndani ya uwezo wao.  Alipoulizwa kuhusu familia ya Mo Dewji kutangaza dau la Sh1bilioni kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo, Masuani amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa si msemaji wa familia. Hata hivyo, amesema wananchi wana nafasi ya kutoa taarifa kwa polisi  ili wawe...

Mbaya wa Yanga alia hali ngumu, " Nakiona cha moto"

Mrundi wa Stand United aliyewapiga Yanga hat trick kwenye Uwanja wa Taifa, Alex Kitenge amekiri kwamba hali yake ni ngumu na anakiona chamoto.  Lakini habari ya kushtua ni kwamba tangu awapige Yanga kwenye mechi iliyomalizika kwa ushindi wa mabao 4-3 Jangwani, hajatumbukiza tena nyavuni mpaka leo.  Kacheza michezo minne bila kufunga hata bao la kuotea kati ya sita waliyocheza Stand.  “Mabeki wengi wamekuwa hawanipi nafasi ya kukaa na mpira nafikiri hii inatokana na kuwafunga Yanga mabao matatu, na kipindi nakuja nilikuwa mgeni wengi walikuwa hawanijui lakini sasa wameshaujua ubora wangu, ila nitajitahidi nirudi kwenye mbio za kuwania ufungaji bora kwa sababu hakuna ligi ambayo nimecheza nikakosa kuwa katika tatu bora ya ufungaji bora,’’ alisema Kitenge

Vigogo Kampuni ya Acacia kortini kwa tuhuma za rushwa

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, kupitia kampuni yake ya North Mara Gold Mine iliyopo mkoani Mara, imeingia katika kashfa baada ya Maafisa Waandamizi wa kampuni hiyo wawili kushtakiwa kwa tuhuma za rushwa ili kupata upendeleo dhidi ya maslahi ya wanavijiji na Serikali ya mkoa huo.  Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Tarime siku ya Jumatano Oktoba 10, 2018 na kusomewa mashtaka ya rushwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.  Kwa nyakati tofauti, watuhumiwa Marteen Van Der, Johannes Jensen, Joseph Kleruu, Bomboga Chikachake, Tanzania O’mtima na Abel Kinyimari wameshtakiwa kwa utoaji na upokeaji wa rushwa wa namna mbalimbali kwa Maafisa wa Serikali na wanasiasa wa mkoani Mara.  Mei 17, 2013 watuhumiwa Marteen Van Der na Johannes Jensen walitoa rushwa ya jumla ya shilingi 93,896,000 kwa Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali Adam Yusuph pamoja na kumpa Peter Mrema 30,000,000 ili kupata upendeleo wak...

Kuna changamoto na athari kubwa sana ukioa mwanamke mzuri

AWALI ya yote naomba niseme kwamba, raha ya ndoa ni kumpata mtu ambaye anajua maisha na anajua mapenzi pia. Ukipata mwanamke ambaye anajua kutafuta pesa tu lakini kwenye ulimwengu wa mapenzi ni limbukeni, atakusumbua sana.  Lakini pia ukijichanganya ukaoa mwanamke ambaye ni mtaalam wa mapenzi lakini hajui pesa inavyotafutwa, nalo ni tatizo licha ya kwamba kwa wengine si tatizo kwani wapo ambao hawataki kuoa wanawake wenye vipato kutokana na yale yanayosemwa kuwa, baadhi yao wakijua kutafuta pesa, wanakuwa viburi.  Hata hivyo, kwa wanaume wanapofikia muda wa kuoa kila mmoja huwa na chaguo lake. Kila mtu atakuwa na vigezo vyake ambavyo vinaweza kutofautiana kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine.  Tofauti hiyo inakuja hata kwenye suala la tabia na uzuri. Kwa mfano, wapo ambao wanaangalia sana suala la tabia nzuri na muonekano mzuri pia. Lakini unaweza kushangaa mwanaume akatafuta mwanamke ambaye anakunywa pombe na anayependa kujirusha kwa kuwa na yeye ni mtu wa mamb...

Fahamu mambo yanayochangia kupoteza hisia za mapenzi

Lipo jambo muhimu analopaswa kuzingatia kila aliye kwenye uhusiano ikiwa anataka kutosheka na penzi la mpenzi wake.  Kwanza ni lazima uitosheleze akili yako, lakini pili, unapaswa kuamini kwamba uliyenaye ni bora na hata ikiwa kuna kasoro, jambo la msingi ni kuzungumza kuondoa tatizo hilo, siyo zaidi.  Anachanganya mambo, hatosheki   Ukweli ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki katika mapenzi ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.  Lakini pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao wa zamani, ambao labda walikuwa wana uwezo mkubwa zaidi katika tendo hilo kuliko sasa.  Hata hivyo, wakati mwingine wanashindwa kuelewa kuwa hata wale wanaofikiri ni wazuri, kama wangekuwa nao hadi leo, huenda wasingeweza kuendelea kuwa imara.  Hii ni kwa sababu, watu wengi baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu hupoteza nguvu au shauku ya tendo hilo.  Zi...

MAMA NA DADA WA CR7 WAJIPANGA KUMTETEA RONALD JUU YA SHUTUMA ZINA MKABIRI

Familia ya Ronaldo yaja juu Familia ya mwanasoka raia wa Ureno na klabu ya Juventus ya Italia, Cristiano Ronaldo, imeshutumu  vikali madai dhidi yake, ambapo dada yake, Katia Aveiro,  na mama yake, Dolores Aveiro,  wame-post picha yake na ujumbe mbalimbali kuhusu suala hilo kwenye mitandao ya Facebook na Instagram.  “Ninataka kumwona mtu aliye na ujasiri wa kuiweka picha hii katika mitandao na kumvunjia heshima… kuivunjia heshima Ureno na umoja wa watu wetu wa kupigania haki,” yalisema maelezo kwenye picha hiyo.  Picha hiyo ina maelezo mengine mawili kwa Kireno, moja ikisema “#Ronaldo, tuko na wewe hadi mwisho” nyingine  “Haki itendeke kwa CR7”.  Ronaldo amefunguliwa mashitaka ya ubakaji na Kathryn Mayorga anayedai alimshambulia katika hoteli moja huko Las Vegas, Marekani,  mwaka 2009. Mayorga aliongeza kwamba Ronaldo alimlipa Dola 375,000 kumtaka asilitangaze jambo hilo.  Nyota huyo wa soka amesema madai hayo ni ya uwongo. ...