Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 08.04.2019: Pochettino, Pogba, Kepa, Giroud, Coutinho

Philippe Coutinho Winga wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho - ambaye kwa sasa yupo Barcelona ya Uhispania- anasema hana mpango wa kurejea kwenye ligi ya Premia. Coutinho, 26, ambaye ni nyota pia wa timu ya taifa ya Brazil alijiunga na Barca Januari 2018. (Mirror) Real Madrid wanatarajiwa kutangaza dau la kumnunua kipa wa Chelsea raia wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 24. (Teamtalk) Chelsea wanataka kumsajili kiungo wa klabu ya Athletico Paranaense ya nchini Brazil Bruno Guimaraes, 21, iwapo watafamikiwa kuchomoka kwenye marufuku ya kufanya usajili. (Mail) Real Madrid wanamatumaini kuwa wakala Mino Raiola atamshawishi mchezaji wake Paul Pogba, 26, ahamie timu yao kutoka Manchester United. (Marca) AC Milan wanamtaka kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino kumrithi Gennaro Gattuso kushika mikoba ya timu hiyo na watampatia kitita cha pauni milioni ili afanye usajili wa wachezaji mwishoni mwa msimu huu. (Mirror) Kablya ya kutua Spurs, Mauricio Pochettino alikuwa meneja wa Espan...

Israel: Isaak Hayik avunja rekodi ya mchezaji soka mkongwe zaidi duniani

Haak Hayik mchezaji soka mkongwe duniani Mchezaji wa soka wa Israel, Isaak Hayik aliye na miaka 73 amevunja rekodi ya kuwa mwanasoka mkongwe zaidi duniani. Isaak aliandikisha historia hiyo baada ya kucheza kama mlinda lango wa timu ya Israeli ya Ironi ama Yehuda siku ya Ijumaa. Licha ya umri wake mkubwa, Hayik alisema "yuko tayari kwa mchezo mwingine" baada ya kucheza kwa dakika 90. Amepokea tuzo ya Guinness World Records katika hafla iliyoandaliwa baada ya mechi hiyo, siku kadhaa kabla ya sherehe 74 ya kuzaliwa kwake. Japo timu yake ilifungwa mabao 5-1 na timu ya Maccabi Ramat Gan, mzaliwa hiyo wa Iraq anasemakana kuwa alionesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo. "Hii sio fahari yangu pekee bali ni fahari ya Israel michezoni kwa ujumla," Hayik aliliambia shirika la habari la Reuters. Mmoja wa watoto wake wa kiume Moshe Hayi, aliye na umri wa miaka 36, alisifia ufanisi wa baba yake kwa furaha na bashasha"siamini kwa kweli", alisema. Haki mili...

Muungano wa G7 na Umoja wa mataifa walaani mapigano mapya Libya

Vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli vimeripotiwa kuungana na serikali kulinda mji mkuu Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani G7, pamoja na Umoja wa mataifa yamelaani vikali mapigano yaliozuka upya nchini Libya. Mataifa hayo yanataka pande zinazohasimiana Libya "kusitisha mara moja shughuli za kijeshi". Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito huo. Tripoli ni makao makuu ya serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa, na ambayo pia inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vikosi vya kulinda usalama vya umoja wa mataifa katika mji huo vimekuwa katika hali ya tahadhari. Ghasia zimekumba Libya tangu utawala kiongozi wa nchi hiyo wa mda mrefu, Muammar Gaddafi kuangushwa na yeye kuuawa mwaka 2011. Nini kinachofanyika ? Kamanda Khalifa Haftar, ambaye ni kiongozi wa vikosi vya kijeshi vinavyopinga utawala wa Tripoli siku ya Alhamisi aliamuru vikosi vyake kuingia mji wa Libya. Hatua hiyo ilijiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Ma...

Waziri wa Uingereza akosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania

Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje wa Uingereza akosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania  Waziri Kivuli wa Mambo ya nje wa Uingereza Liz McInnes aimeikosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje wa Uingereza ameeleza kusikitishwa kwake na kupitishwa kwa sheria ya vyama vya siasa nchini Tanzania ambayo anadai inaminya vyama vya upinzani. Liz McInnes ambaye ni mbunge kupitia chama cha upinzani Labour amekaririwa na  mtandao wa chama chake akisema wapinzani inabidi waachiwe uhuru wao . ''Inasikitisha kusikia kuwa bunge la Tanzania limepitisha sheria ambayo inazuia vikali shughuli za kisiasa na kutoa mamlaka kwa msajili wa vyama vya siasa kuvifutia usajili vyama vya upinzani''. ''Wanasiasa wa upinzani wanapaswa kuwa na uhuru wa kuipa changamoto serikali na si kuhofia kufungwa kwa kutoa maoni yao ikizingatiwa kuwa kuna chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzji mkuu mwakani''. Mwanasiasa huyo ametahadharisha kuwa mat...

Mo Dewji atuma salaam Al Ahly, Esperance na Mamelodi

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa klabu hiyo itashindana na timu kubwa barani Afrika msimu ujao katika dirisha la usajili. Mohamed Dewji Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe Jumamosi hii, Mo Dewji amesema kuwa bajeti ya klabu hiyo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku huku kutokana na kukamilika kwa mabadiliko ya mfumo wa kiuendeshaji na kupanuka kwa vyanzo vya mapato ya klabu. " Mwaka juzi ukilinganisha na mwaka jana, bajeti yetu imekuwa ikizidi kwa asilimia 60 hadi 70 na mwaka huu bajeti unazidi. Kwakuwa mabadiliko yamefanyika vizuri, tumeanza kupata vyanzo vingi vya mapato ", amesema Mo. " Kiujumla tumejitayarisha kushindana na hizi klabu kubwa na kusajili wachezaji wazuri. Tayari kuna kamati maalum ambayo inalifanyia kazi suala la usajili, kuna wachezaji wengi mikataba yao inaisha. Wengi tutaendelea nao na wengine tutawaacha. Kwahiyo tutakuwepo kwenye ...

Mvulana wa miaka 9 amuoa msichana wa miaka 6 baada ya kuchumbiana kwa miaka mitano Uganda

Wakaazi wa kijiji cha Nakapyata, wilayani Buyende nchini Uganda wamefanya sherehe ambapo watoto wawili walio kati ya umri wa miaka tisa na sita waliozwa katika utamaduni wa kushangaza. Kulingana na mtandao wa gazeti la  Daily Monito r nchini Uganda Uganda, mvulana huyo ambaye yuko katika darasa la nne katika shule ya msingi ya Buyende na msichana ambao wote waliripotiwa kuzaliwa na meno mawili waliozwa siku ya Jumatatu na kupatiwa nyumba ya kitamaduni kuishi. Chini ya sheria za Uganda , ni makosa kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 kufunga ndoa ama hata kushiriki katika tendo la ngono. Inadaiwa kuwa watoto hao wawili walianza kuchumbiana wakati mvuana alipokua na miaka mitatu na msichana akiwa na umri wa miezi mitatu pekee. Hatua hiyo baadaye iliimarisha uhusiano kati ya familia zote mbili , huku Delifazi Mulame babake mvulana akimuita msichana huyo kama 'mke wa mwanangu'. ''Mwanangu alizaliwa na meno mawili na mkewe akazaliwa na meno mawili. Kuzaliwa kwak...

Mvulana wa miaka 9 amuoa msichana wa miaka 6 baada ya kuchumbiana kwa miaka mitano Uganda

Wakaazi wa kijiji cha Nakapyata, wilayani Buyende nchini Uganda wamefanya sherehe ambapo watoto wawili walio kati ya umri wa miaka tisa na sita waliozwa katika utamaduni wa kushangaza. Kulingana na mtandao wa gazeti la  Daily Monito r nchini Uganda Uganda, mvulana huyo ambaye yuko katika darasa la nne katika shule ya msingi ya Buyende na msichana ambao wote waliripotiwa kuzaliwa na meno mawili waliozwa siku ya Jumatatu na kupatiwa nyumba ya kitamaduni kuishi. Chini ya sheria za Uganda , ni makosa kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 kufunga ndoa ama hata kushiriki katika tendo la ngono. Inadaiwa kuwa watoto hao wawili walianza kuchumbiana wakati mvuana alipokua na miaka mitatu na msichana akiwa na umri wa miezi mitatu pekee. Hatua hiyo baadaye iliimarisha uhusiano kati ya familia zote mbili , huku Delifazi Mulame babake mvulana akimuita msichana huyo kama 'mke wa mwanangu'. ''Mwanangu alizaliwa na meno mawili na mkewe akazaliwa na meno mawili. Kuzaliwa kwak...