Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Spika Ndugai ataja kosa kubwa analoshtakiwa Masele

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele, hawezi kukaidi tena agizo la kutakiwa kufika Kamati ya Maadili baada ya kuitwa na Spika huyo kwa mara ya pili. Spika wa Bunge Job Ndugai. Akizungumza na waandishi wa habari Spika Ndugai amesema suala la Bunge kumuita Masele halihusiani na matukio yaliyotokea Afrika Kusini bali ni kwa sababu ya mambo aliyofanya nyumbani. Spika Ndugai amesema " ameitwa kwa mambo ya hapa nyumbani ya utovu wa nidhamu, anaunganisha hilo na matendo anayoyafanya huko, lakini hatujamuita kwa mambo ya South Afrika Watanzania watulie baada ya muda zitaletwa bungeni kila mtu atasikia kuhusu anatuhumiwa nini na majibu yake yalikuwa nini na wataelewa kama ameonewa au hajaonewa ." " Stephen Masele hawezi kukaidi zaidi kwa sababu ni lazima arudi Tanzania, labda sababu awe mkimbizi na  akirudi Tanzania lazima aje Kamati ya Maadili, ni wito wa kisheria tunachomuitia ni tabia yake uchonganishi wa viongozi, kwa sasa hatu...

Mwalimu kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa

Mwalimu kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa Taassis ya kuzuaia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara inatarajia kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Masasi, Mwanaid Abdalah Mtaka kwa tuhuma za kutumia nyaraka za uongo na kujipatia fedha kiasi cha Shilingi 1,578,000. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Takukuru Mkoani humo, Stephen Mafipa , amesema kuwa Mtaka anakabiliwa na kosa la jinai kwa kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake kisha kujipatia kiasi hicho cha fedha jambo ambalo ni kinyume na sheria. “Alitumia na kuwasilisha stakabadhi zenye kuonyesha alitumia jumla ya shilingi 1,578,000/= kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya shule ya Msingi Masasi, hukub akijua kwamba hakununua,”Amesema Mafipa. Aidha, kitendo hicho kilimuwezesha mtuhumiwa kujipatia kiasi cha shilingi 1,578,000/= ambazo alizitumia kwa matumizi yake binafsi. Kesi hiyo ya Jinai itafunguliwa katika mahakama ya wilaya...

Sababu 5 kwanini wasanii Tanzania hupenda kuoa nje

Alikiba na AY wakiwa na wake zao Wasanii kama Alikiba, Ben Pol na AY, wote wamefanikiwa kuoa nje ya nchi, huku Ben Pol akiwa mbioni kumuoa mpenzi wake Anerlisa ambaye ni raia wa Kenya baada ya kumvisha pete ya uchumba hivi karibuni. Alikiba pia ameoa Kenya na AY amemuoa mrembo raia wa Rwanda. Mwijaku ambaye ni muigizaji maarufu nchini na mtu maarufu katika mitandao ya kijamii, amezitaja sababu 5 zinazopelekea wasanii wa Tanzania kuamua kuoa nje ya nchi. Sababu ya kwanza ameitaja kuwa ni uoga wa wasanii wa kiume maarufu Tanzania, kutokana kuwa wanahisi wanawake wa Kitanzania wanawafahamu nje ndani. Sababu ya pili ni kuogopa kuchaguliwa au kukosolewa uchaguzi wa wanawake wao na ndugu wa familia. Mtazame hapa chini Mwijaku akielezea zaidi sababu hizo

Masele: Natii wito wa Ndugai, nataka kujua mambo ya hovyo hovyo nayoyafanya

Natii wito wa Ndugai, nataka kujua mambo ya hovyo hovyo nayoyafanya- Masele Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (Pan- African Parliament – PAP), Steven Masele amesema kuwa ameamua kuitikia wito wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ili kuweza kujua ni mambo gani ya hovyo hovyo anayoyafanya. Ameyasema hayo wakati akizungumza na DW ambapo amedai kuwa yeye alikuwa akitimiza majukumu yake ya kuongoza kamati maalum ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili rais wa bunge la Afrika, Nkodo Dang. Amesema kuwa anarejea nyumbani Tanzania ili kuitikia wito huo na kutaka yawekwe wazi kwa wananchi hayo mambo ya hovyo hovyo anayoyafanya huko Afrika Kusini sehemu ambayo ni kituo chake cha kazi. ”Nimemsikiliza Spika wangu Job Ndugai sijamuelewa, niko njiani narudi nyumbani Tanzania kuweza kujua hayo mabo ya hovyo hovyo ninayoyafanya ni yapi, na pale nilikuwa natekeleza majuk...

AFCON: CAF YA TANGAZA BEI ZA KUONA MCHEZO HUKO MISRI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali za Africa (AFCON) zinazotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri. Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike aliyebebwa na wachezaji. Shrikisho la soka nchini TFF limethibitisha taarifa hiyo, ikisema kuwa CAF imetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali. Kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la kwanza ni USD 29 ambayo ni sawa na takribani sh 66,700 za Kitanzania, tiketi za daraja la pili ni USD 18 ambazo ni sawa na sh 41,403 tiketi za daraja la tatu ni USD 6. Katika hatua ya makundi, Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja la kwanza ni  USD 35 ambayo ni takribani sh 80,521 kwa daraja la pili ni USD 24 na daraja la tatu ni ...

Kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Awad Ibn Auf kwanini amejiuzulu

Bwana Ibn Auf ameondoka madarakani siku moja baada ya kuwa mkuu wa baraza la jesi Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baaba ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Waziri wa ulinz Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan. jeshi limesema kuwa litaendelea kuwa madarakani kw amiaka miwili na baadae utafanyika uchaguzi. Lakini viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia. Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007. James Copnal...

Mzozo Sudan: Baraza la kijeshi lawakamata waliokuwa maafisa wa serikali

Raia Khartoum wameapa kuendelea na maandamano mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan limewakamata waliokuwa maafisa wa serikali na kuahidi kutowatawanya waandamanaji. Msemaji mmoja pia ameuomba upinzani kumchagua waziri mkuu mpya na kuahidi kumuidhinisha watakayemchagua. Maandamano ya miezi kadhaa nchni Sudan yamechangia kutimuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini Sudan Omar al-Bashir Alhamisi wiki iliyopita Waandamanaji wameapa kusalia mitaani mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia Raia wanaendelea kuandamana na wamekita kambi nje ya makao makuu ya wizara ya ulinzi katika mji mkuu Khartoum. Je baraza la kijeshi limesema nini ? Katika mkutano na waandishi habari siku ya Jumapili, msemaji Meja Jenerali Shams Ad-din Shanto ameeleza kwamba baraza la kijeshi lipo "tayari kuidhinisha" serikali yoyote ya kiraia itakayoidhinishwa na vyama vya upinzani. "Hatutomteua waziri mkuu. Watamchagua," alisema akimaanisha upinzani...