Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

MAHAKAMA MOJA NCHINI UFARANSA IMEANZA KUSIKILIZA KESI YA KUKU

Ufaransa: Jogoo Maurice afikishwa mahakamani kwa kuwapigia watu kelele anapowika Sambaza habari hii Messeng ambaza habari hii Tw Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha P Image caption Mmiliki wake, Corinne Fesseau, anasema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote wanafanya 'kuwikaa' Jogoo huyu ambaye mmiliki wake amempatia jina la Maurice, amekuwa kero kwa majirani kwa kuwika kila alfajiri na malambuna kumhusu sasa yanajadiliwa katika mahakama moja nchini Ufaransa. Analaumiwa kwa kusababisha kalele na familia moja katika kisiwa cha Oléron huko Ufaransa. Mmiliki wake, Corinne Fesseau, anasema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote wanafanya 'kuwikaa'. Waliomshtaki Maurice na Maurice mwenyewe hawakufika mbele ya mahakama ya mji wa magharibi wa Rochefort siku ya Alhamisi kesi ilipoanza kusikilizwa. Lakini jogoo huyo ambaye amekuwa maarufu kutokana na kesi inayomkabili, amepata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama. Haki mi...

MTANZANIA AHUKUMIWA KWENDA JELA MAISHA KENYA

: Mahakama jijini Nairobi imewahukumu washukiwa watatu wa ugaidi nchini Kenya waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio la mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa. Miongoni mwa waliohukumiwa ni Rashid Charles Mbeserero anayetuhumiwa kuhusika katika shambulio hilo ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, wengine waliohukumiwa na Mtanzania huyo ni  Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar ambao wao wamehukumiwa kwenda jela miaka 41 kila mmoja. Wote walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa wanachama wa Kundi la Al-Shabab.Takriban wanafunzi 148 walifariki dunia katika shambulio hilo. Hukumu hiyo imepitishwa baada ya mahakama kujiridhisha kuwa watatu hao ni wanachama wa Kundi la Al-shabab kutoka Somalia

Tetesi za Soka Ulaya na Afrika Jumatano 03.07.2019: Maguire, Bale, Lacazette, Cocu, Ajibu, Dembele

Alexandre Lacazette Atletico Madrid wanataka kumsajili Alexandre Lacazette kuchukua nafasi ya mshambuliaji Antoine Griezmann, 28 ambaye anaelekea Barcelona. (Mirror) United watalazimika kilipa zaidi ya pauni milioni £90 kumnunua beki wa Leicester City na England, Harry Maguire - hatua itakayomfanya kuwa nyota huyo wa miaka 26 kuwa mlinzi ghali zaidi . (Telegraph) United pia imetuma maombi ya kumnasa kiungo wa kati wa Uhispania na Dinamo Zagreb-Dani Olmo, 21. (Mail) Real Madrid wana mpango wa kumjumuisha mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, katika mkataba utakaowawezesha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mail) Gareth Bale Mlinzi wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24, huenda akatia saini mkataba wa kujiunga na Manchester City mhumu ujao. (L'Equipe, via Manchester Evening News) Crystal Palace wanafanya kila juhudi kuhakikisha hawataiuzia Arsenal winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, na wana hasiri kwa sababu wanaamini G...

Ndege apigwa picha akimpatia kinda kipande cha sigara

Mpiga picha za wanayamapori amepiga picha ya Ndege mmoja aliyekuwa akilisha kinda wake kipande cha sigara kilichobaki baada ya kutumika, katika ufukwe mjini Florida nchini Marekani. Katika ukurasa wa Facebook, Karen Mason amesema aliwaona ndege hao mwezi uliopita. Alisema: ''kama utavuta sigara, tafadhali usiache mabaki ya sigara.'' Taasisi ya kutunza mazingira ya hifadhi nchini Uingereza imesema picha hiyo ''inasikitisha''. Bi Mason alipiga picha nyingine ya kinda akiwa amebeba kipande cha mabaki ya sigara mdomo wake: KAREN MASON Ndege hufanya makosa kuwalisha makinda vipande vya sigara kwa kudhani ni chakula. ''Ndege wengi wana shauku kuhusu vitu ambavyo tunavitupa, na mara nyingi huchunguza kwa kuvijaribu ili kujua kama ni chakula au la,'' msemaji wa taasisi ya kulinda ndege aliiambia BBC. ''inasikitisha, mzazi huyu ameamua kuwa mabaki ya sigara kuwa kitu cha kumlisha kinda wake. ''Viumbe hawa wanajaribu ...

Waabiri ndege kisiri 'stowaway' huponea?

Mshukiwa aliyeabiri ndege kisiri inaaminika ameanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways  kutoka Nairobi kuelekea Heathrow, na kuanguka katika bustani moja huko kusini mwa London Lakini ni mara ngapi visa kama hivyo huhuhudiwa na hali huwa vipi wakati wa safari za aina hiyo? Ni mara ngapi visa hivi hutokea? Licha ya kwamba sio jambo la kawaida, hii sio mara ya kwanza kwa mtu kuingia katika sehemu za ndege wakati ndege hiyo ikisafiri na kujificha wakati wa safari ya kuelekea Uingereza. mwili ulipatikana katika bustani ilioko Offerton Road huko Clapham Kati ya Januari 2004 na Machi 2015, watu sita walioingia kwa siri katika ndegekatika uwanja wa ndege Uingereza walipatikana kwa mujibu wa  takwimu za hivi karibuni za shirika la viwanja vya ndege (CAA ). Mwingine mmoja alipatikana katika ndnai ya ndege ya Uingereza katika uwanja wa ndege ng'ambo. Takwimu kutoka shirika la viwanja vya ndege Marekani zimeashiria kuwa watu 96 wamewahi kujificha katika sehemu za ndege ...

NDEGE YA KENYA YA DODOSHA ABIRIA UINGEREZA

Mwili wa mtu aliyeabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' waanguka London ''Mtu'' huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi Jumapili mchana Mwili wa mtu anayeshukiwa kuabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' umeanguka ndege hiyo ikielekea kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London. Mwili huo - unaoaminiwa kuwa wa mwanamume - ulipatikana umeanguka katika bustani ya Clapham siku ya Jumapili. Polisi wanasema mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi. Mkoba, maji na vyakula vilipatikana katika eneo lililo chini ya gia ya ndege wakati ilipokua ikutua. Polisi wa wa jiji la London wamesema mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake na kwamba kifo chake. Kenya Airways imesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilefu yoyote ilioripotiwa. Msemaji wa shirika la ndege hiyo amesem...

Kim Kardashian West aachana na jina la Kimono kufuatia ghadhabu za raia wa Japani

Kim Kardashian West anajipanga kubadilisha jina la nguo zake za ndani kufuatia shutuma kali za kudunisha mila. Raia wa Japani wanaotumia mitandao ya kijamii walishutumu vikali jina la kibiashara la nguo hizo, Kimono. Kimono ni jina la vazi la taifa na kitamaduni nchini Japani. Awali Bi Kardashian, alijitetea na kusema hatobadili jina hilo, akisema halikuwa lengo lake kukashifu vazi au utamaduni wa jamii fulani. Lakini leo Jumanne, amesema kuwa atatangaza jina lengine la nguo hizo hivi karibuni. Ruka ujumbe wa Instagram wa kimkardashian Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa kimkardashian Nyota huyo wa Televisheni, mwanamitindo na mbunifu wa mavazi ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa: "Kila siku nasikiliza watu, najifunza na kukua… Nilipotangaza jina la nguo zangu, nilifanya hivyo nikiwa na nia njema moyoni." Kimono ni vazi rasmi nchini Japani toka Karne ya 16 Ameongeza: "Baada ya kulifikiria kwa kina, nitazizindua tena kwa jina jipya." Ki...