ARSENAL YATAKATA KWA REKODI UINGELEZA

MTEULE THE BEST

Ni muda wa kuweka historia katika mchezo huu wa soka na nyingi zikitoka kwa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi haswa kila wanachofanya hawa watu zinakuwa rekodi , lakini sasa rekodi nzuri imehamia kwa Arsenal ya pale England mara baada ya kushinda mechi nyingi mfululizo.


Timu hiyo imecheza michezo 23 kwa kipindi cha hivi karibuni kwa mashindano yote na imebahatiba kufungwa mchezo mmoja ambao ule wa Liverpool katika ufunguzi wa ligi kuu England EPL baada ya hapo katika michezo hiyo 23 wametoa sare 6 huku wakishinda michezo 16 na kupata ‘Clean Sheet’ 14.

Magoli yaliyofungwa katika michezo hiyo ni 53 huku wakiruhusu magoli 16 kwa takwimu hizo inaonesha kuwa timu hiyo iko katika wakati mzuri kwa kipindi hiki, mashaka kwa wapenzi na mashabiki wa Arsenal huu mwezi tunaouingia ndio mwezi wao wa majeruhi kama wakiuvuka vizuri basi itakuwa ahueni kwao , maana kila mwaka ndio mwezi ambao unawasumbua sana kwa kupata wachezaji majeruhi.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU