WANAMITINDO WANAOINGIZA MKWANJA MREFU

MTEULE THE BEST

Tasnia ya urembo imekuwa ikitoa ajira kwa wasichana wengi na wengine hufanikiwa kimaisha kutokana na kazi hiyo, MTEULE THE BEST inakuletea orodha ya wanamitindo tatu bora wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi duniani.

Gisele Bundchen

Mrembo huyu alizaliwa Brazil mwaka 1982, ni mwanamitindo pekee aliyefanikiwa na kuwa maarufu kwenye miaka ya 90 na mwaka 2011 aliingia kwenye orodha ya wanawake matajiri ulimwenguni akishikilia namba 16, kwa mwaka mrembo huyu analipwa dolla milioni 44.

Doutzen Kroes

Mrembo huyu alizaliwa mwaka 1985 mbali na kuwa mwanamitindo pia ni muigizaji maarufu nchini Netherland, ambapo aliwahi kuwa mtangazaji  wa Victoria’s TV show huko New York na kwa mwaka anaingiza zaidi ya dola milioni tisa kutokana na kazi yake ya uanamitindo.

Adriana Lina

Mrembo huyu alizaliwa mwaka 1981 huko nchini Brazil, tofauti na mitindo anajishughulisha pia na uigizaji pia aliwahi kushinda nafasi ya pili kwenye mashindano ya Ford Super Model of the World, kwa mwaka anaingiza dola milioni 9 na zaidi.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU