Kifo cha Nkaissery: Matiang'i ateuliwa kaimu waziri wa usalama Kenya

MTEULE THE BEST


Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa usalama wa ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery.
Waziri huyo wa usalama alifariki dunia muda mfupi baada ya kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen jijini Nairobi kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Uteuzi wa Dkt Matiang'i umetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuongoza mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama wa Taifa.
Waziri wa usalama Kenya Nkaissery afariki dunia
Rais Kenyatta amesema hakutakuwa na pengo lolote kiusalama nchini kutokana na kifo cha jenerali huyo mstaafu.
Rais amesema maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 Agosti, mwezi mmoja kuanzia sasa, yataendelea bila kuvurugika.
Bw Kenyatta amewataka Wakenya kuendelea kudumisha utulivu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU