MTEULE THE BEST Image caption Ramani ya Ethiopia Umoja wa mataifa unataka Ethiopia kuruhusu waangalizi wa kimataifa kuingia katika maeneo ambayo hivi majuzi yaliathirika na maandamano yenye ghasia nchini humo. Mkuu wa shirika la haki za binadamu laumoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein anasema hakujakuwa na jaribio la kuchunguza ghasia hizo au kumpata mhusika. Image copyright AFP Image caption Maelfu ya watu waliandamana dhidi ya sera ya serikali kuwapokonya ardhi Shirika la haki za binadamu la kimataifa Amnesty International linasema kuwa takriban watu 100 waliuawa kwenye maandamano katika maeneo ya Oromia na Amhara mwishoni mwa wiki. Image caption Waethiopia wazika waliouawa katika maandamano Jumapili ilishuhudia makabiliano makali baina ya waandamanaji na maafisa wa utawala. Waandamanaji hao walikuwa wakipinga sera mpya ya serikali ya kupanua jiji la Addis Ababa ambayo ililazimu baadhi yao kupokonywa ardhi. Kulishuhudiwa pia maandamano makubwa katika eneo la Oro...