Gazeti la Mseto nje kwa miaka 3

MTEULE THE BEST

Tanzania imelipiga marufuku gazeti la Mseto
Image captionGazeti la Mseto lafungwa kwa miaka 3
Serikali nchini Tanzania imelifungia gazeti la kila wiki la Mseto kuchapishwa katika njia zote ikiwa ni pamoja na mitandao. Hili ni gazeti la pili kufungiwa ndani ya mwaka mmoja.
Serikali inasema Mseto limekuwa likiandika taarifa za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za serikali huku taarifa hizo zikiwa na nia ya uchochezi na kumchafua Rais John Magufuli na viongozi wengine wa serikali yake.
Akitangaza kufungiwa kwa gazeti hili mapema leo hii, Waziri mwenye dhamana ya habari Nape Nnauye amewaambia waandishi wa habari kuwa amelifungia gazeti hilo kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976
Hakuna taarifa rasmi yoyote ya mwitikio wa kufungiwa huko kutoka kwa wachapishaji na wamiliki wa gazeti hilo
Hili ni gazeti la pili kufungiwa ndani ya mwaka mmoja. Mwezi Januari mwaka huu, serikali ililifungia pia gazeti la Mawio muda wote.
Wasiwasi miongoni mwa wadau wa habari umeendelea kuongezeka kwa kile kinachoonekana kuwa utawala huu mpya unaviminya vyombo vya habari na kukandamiza uhuru wa kutoa na kupokea habari pia hapa nchini Tanzania.
Tayari watu wawili wameshtakiwa baada ya kuandika jumbe katika mitandao ya kijamii zilizoonekana kumtusi Rais Magufuli
Serikali ya Tanzania imelifungia nje gazeti la Mseto kwa miaka 3
Image captionTanzania: Gazeti la Mseto nje kwa miaka 3
Inawezekana kufungwa huku kwa gazeti la Mseto kutaibua ukosoaji hasa kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakiikosoa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo wanasema inatoa mamlaka makubwa sana kwa serikali kuminya uhuru wa habari nchini

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU