Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Simu milioni 900 za Android hatarini

MTEULE THE BEST


Simu ya kisasa ya Android
Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani.
Upungufu huo unaowapa wadukuzi mlango wa nyuma wa kuiga herufi za siri uligunduliwa baada ya watafiti wa hali ya ubora wa programu Checkpoint walipojaribu kusuluhisha hitilafu iliyowezesha kirusi kuambukiza makumi ya mamilioni ya simu zilizokuwa na programu zilizoundwa na kampuni moja ya Marekani Qualcomm.
Kampuni hiyo inayounda programu za simu imeuza programu hiyo kwa watengenezaji wa simu milioni 900.
Hilo linamaanisha kuwa simu milioni 900 zipokatika hatari kubwa ya kudhibitiwa na wadukuzi.

Aina ya simu zilizoathirika

  • BlackBerry Priv na Dtek50
  • Blackphone 1 na Blackphone 2
  • Google Nexus 5X, Nexus 6 na Nexus 6P
  • HTC One, HTC M9 na HTC 10
  • LG G4, LG G5, na LG V10
  • New Moto X ya Motorola
  • OnePlus One, OnePlus 2 na OnePlus 3
  • Samsung Galaxy S7 na Samsung S7 Edge
  • Sony Xperia Z Ultra
Mkuu wa kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa programu katika kampuni ya Checkpoint Michael Shaulov, anasema kuwa
''hakuna ushahidi kuwa tayari simu hizo zimeathirika ila kwa mtizamo wetu ni kuwa mlango uko wazi kabisa mtu yeyote mwenye ufundi na ubora kama wangu hivi anafahamu waziwazi kuwa hakuna hata kizingiti cha kumuibia mtu herufi za siri katika simu hizo tulizotaja hapo juu''
AndroidImage copyrightAP
Image captionUpungufu unamwezesha mtu wa tatu kumpokonya mmiliki wa simu udhibiti kwani anaweza hata akabadilisha herufi za siri bila yako wewe kujua.
''upungufu unamwezesha mtu wa tatu kumpokonya mmiliki wa simu udhibiti kwani anaweza hata akabadilisha herufi za siri bila yako wewe kujua''
''Ni hatari sana , ni kama mtu amejenga nyumba akaweka mle ndani mali ya thamani ya juu kisha akaondoka akiwa ameacha mlango wake wazi''alisema Shaulov.
Checkpoint tayari imeanza kutoa programu zenye uwezo wa kudhibiti simu hizo na tayari wameipa kampuni ya Qualcomm mbinu za kudhibiti simu hizo.
Njia moja ya kuimarisha usalama wa simu wanasema ni kununua programu kutoka kwa soko maalum la Google Play.
Qualcomm imenyamaza kimya kuhusu ripoti hii iliyotolewa na Checkpoint.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...