Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wafahamu vijana 10 wa chini ya miaka 30 walio matajiri zaidi duniani

MTEULE THE BEST

Hugh Grosvenor

Image copyrightGETTY IMAGES
Tajiri mmiliki wa ardhi ambaye pia amekuwa akisaidia wasiojiweza katika jamii, Mtawala wa Westminister Gerald Cavendish Grosvenor amefariki na kumwachia mwanawe Hugh Grosvenor urithi wa £9bn.
Alikuwa na binti watatu, na mwana mmoja pekee wa kiume, Hugh, mwenye umri wa miaka 25.
Hugh amerithi "nusu ya London" kwani ardhi nyingi maeneo mengi ya Belgravia na Mayfair, London ilimilikiwa na babake.
Yeye hufanya kazi katika kampuni ya Bio-bean, kampuni inayoangazia teknolojia isiyoongeza gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani.
Kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes ya mwaka 2016, kuna vijana wengine tisa wa chini ya umri wa miaka 30 ambao utajiri wao ni zaidi ya dola bilioni moja za Marekani.
Vijana wengine matajiri ni:
2 & 3: Alexandra, 20, na Katharina Andresen, 21
Ndio wachanga zaidi na wanamiliki kampuni ya Ferd.
Binti hawa walirithi utajiri hu kutoka kwa baba yao Johan, raia wa Norway mwaka 2007.
4: Gustav Magnar Witzoe, 23
Anatoka Norway pia na huonesha maisha yake ya kifahari kwenye Instagram.
Amerithi sehemu ya biashara ya babake ya kufuga samaki na sasa utajiri wake ni $1.1bn (Ā£846m).
Gustav Witzoe, babake ambaye wana jina sawa, alimpa hisa kwenye kampuni hiyo kama zawadi. Lakini hana udhibiti au usemi wowote.
5&6: Ludwig Theodor Braun na dadake
Haonekani sana mtandaoni. Hayupo kwenye Twitter au Instagram lakini anatambuliwa kwa utajiri.
Familia yake ilianzisha kampuni ya dawa ya B. Braun Melsungen, Ujerumani 1839.
Kampuni hiyo ni maarufu sana kwa dawa na vifaa vya matibabu.
Ludwig humiliki 10% ya kampuni hiyo ambayo ni sawa na $1.8bn (Ā£1.4bn).
Dadake Eva Maria Braun-Luedicke yuko nyumba yake kidogo lakini utajiri wake ni $1.4bn (Ā£1bn).

7&8: Waanzilishi wa Snapchat

Waanzilishi wa Snapchat Evan Spiegel na Bobby MurphyImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWaanzilishi wa Snapchat Evan Spiegel na Bobby Murphy
Evan Spiegel ni mmoja wa walioanzisha mtandao wa Snapchat ambao hutumiwa na mamilioni ya vijana duniani.
Majuzi, aliingia uchumba na mwanamitindo mashuhuri duniani Miranda Kerr.
Evan Spiegel na Miranda KerrImage copyrightGETTY IMAGES
Ana umri wa miaka 26 na utajiri wake ni $2.1bn (Ā£1.6bn), Evan ndiye mchanga zaidi miongoni mwa waanzilishi wa Snapchat na ndiye tajiri zaidi miongoni mwao.
Mwenzake ni Bobby Murphy, 28, ambaye anamkaribia sana kwa utajiri.
Utajiri wa Murphy ni $1.8bn (Ā£1.3bn).
9: Lukas Walton
Kwa mujibu wa Forbes, Lukas Walton, 29, ndiye anayemkaribia sana Hugh Grosvenor, 29.
Utajiri wake ni $10.4bn, ambazo ni karibu £7.2bn kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji wa fedha vya sasa.
Anatoka katika familia tajiri inayomiliki Walmart (miongoni mwa kampuni nyingine), ambayo pia humiliki Asda nchini Uingereza.
10: Wang Han
Wang Han, raia wa China, anakamilisha orodha hii.
Chanzo cha utajiri wake ni urithi wa hisa za kampuni ya ndege ya Juneyao Air kutoka kwa babake Wang Junyao, aliyefariki 2004.
Junyao alikuwa mwanzilishi wa kampuni ya Juneyao Group. Wang Han humiliki 27% ya hisa za shirika hilo la ndege na 14% ya hisa za maduka ya jumla ya Wuxi Commercial Mansion Grand Orient.
Utajiri wake unakadiriwa na Forbes kuwa $1.34bn.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...