UN kuchunguza mauaji Oromia na Amharia Ethiopia

MTEULE THE BEST

Watu kadhaa wameuawa kufuatia makabiliano baina ya polisi na waandamanaji
Image captionRamani ya Ethiopia
Umoja wa mataifa unataka Ethiopia kuruhusu waangalizi wa kimataifa kuingia katika maeneo ambayo hivi majuzi yaliathirika na maandamano yenye ghasia nchini humo.
Mkuu wa shirika la haki za binadamu laumoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein anasema hakujakuwa na jaribio la kuchunguza ghasia hizo au kumpata mhusika.
Jamii ya Oromo imekuwa ikilalamikia kutoweka kwa vijana mbali na kukamatwa kwa wengine na maafisa wa usalamaImage copyrightAFP
Image captionMaelfu ya watu waliandamana dhidi ya sera ya serikali kuwapokonya ardhi
Shirika la haki za binadamu la kimataifa Amnesty International linasema kuwa takriban watu 100 waliuawa kwenye maandamano katika maeneo ya Oromia na Amhara mwishoni mwa wiki.
Raia wa Ethiopia wazika jamaa zao waliouawa katika makabiliano na polisi
Image captionWaethiopia wazika waliouawa katika maandamano
Jumapili ilishuhudia makabiliano makali baina ya waandamanaji na maafisa wa utawala.
Waandamanaji hao walikuwa wakipinga sera mpya ya serikali ya kupanua jiji la Addis Ababa ambayo ililazimu baadhi yao kupokonywa ardhi.
Kulishuhudiwa pia maandamano makubwa katika eneo la Oromia ambako kunaaminika kuwa watu kadhaa waliuawa.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU