Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wazambia wamchagua Rais mpya

MTEULE THE BEST

Tokeo la picha la zambia
Wazambia wanapiga kura katika uchaguzi wa uraisi na bunge katika kile kinachotarajiwa kuwa ushindani mkali kati ya chama tawala cha Patriotic Front na chama kikuu cha upinzani cha United Party for National Development.
Wapiga kura wa Zambia wakusubiri kutoa sauti zao
Rais wa Zambia Edgar Lungu na mpinzani wake mkuu Hakainde Hichilema wote wamesema wana imani wataibuka washindi katika uchaguzi huo. Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa kumi na mbili asubuhi huku milolongo mirefu ya watu ikishuhudiwa katika vituo hivyo.
Baada ya kukamilika kwa kipindi cha kampeni kilichoghubikwa na vurugu, Lungu na Hichilema waliwatolea wito wapiga kura kujitokeza kwa wingi kupiga kura kila mmoja akiahidi kuuimarisha uchumi wa taifa hilo ambao unasuasua.
Wafuasi wa chama tawala PF na wa UPND walikabiliana wakati wa kampeini na kusababisha hata tume ya uchaguzi kusitisha kampeini hizo kwa muda.
Upande wa upinzani umekuwa ukisumbuliwa
Rais anaemaliza wadhifa wake Edgar Lungu
Wazambia wanakabiliwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira baada ya kufungwa kwa migodi ya madini ya shaba, kupotea mara kwa mara kwa umeme na kupanda kwa bei za vyakula na mahitaji ya kimsingi.
Mbali na kumchagua rais, wabunge na madiwani, raia wa Zambia pia wanapiga kura ya maoni ya kuifanyia mageuzi katiba ya nchi hiyo.
Mgombea urais atahitaji kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura ili kuepusha duru ya pili ya uchaguzi, iwapo sivyo, duru hiyo ya pili itahitaji kufanyika katika kipindi cha siku 37 baada ya uchaguzi huu wa Alhamisi.
Matokeo kamili ya uchaguzi huo mkuu yanatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa au Jumamosi.
Nchi ya Zambia tofauti na nchi zingine za jirani kama vile Angola na Zimbabwe haijaingia katika vita na machafuko makubwa tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1964 ambapo mwaka 2011 kulifanyika uchaguzi wa amani ambao ulimuweka Michael Sata kuwa rais wa nchi hiyo mpaka mwaka 2014 alipofariki na mwaka 2015 kufanyika uchaguzi mwingine uliomuweka Edgar Lungu kuwa raisi wa nchi hiyo ili kumalizia muhula ulioachwa na Rais Sata.
Mara kwa mara Hichilema amekuwa akishutumiwa na maafisa kuwa anapuuzia mashambulizi ambayo yanafanywa na wafuasi wake na mara kadhaa amekamatwa na nyumba yake kuzingirwa na polisi.
Hali ya uchumi ni dhaifu
Ukosefu wa umeme na maji ni miongoni mwa shida nchini Zambia
Chama hicho cha upinzani kinakishutumu chama cha PF kwa kushindwa kudhibiti msukosuko uliosababishwa na kuanguka kwa bei ya madini ya shaba ambayo ndio yenye kuzalisha pato kuu la taifa na ukame uliopelekea uhaba wa umeme mambo yaliosababisha kushuka thamani kwa sarafu ya kwacha na kupanda kwa gharama za maisha.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...