MTEULE THE BEST
Katika utabiri wao, wachambuzi hao ambao ni Thierry Henry, Gary Neville na Jamie Carragher wameiondoa kabisa Leicester katika kinyangāanyiro hicho.
Badala yake, wametupia karata yao ya ubingwa kwa vilabu vya jiji la Manchester. Kitu ambacho kimsingi si cha kushangaza, ukizingatia namna walivyofanya usajili wao kuanzia makocha mpaka wachezaji.
THIERRY HENRY
- Man City 2. Man Utd. 3. Chelsea 4. Arsenal
āSiku zote matumaini yangu yapo kwa Arsenal. Lakini nadhani ubingwa utachukuliwa na kati ya City au United. Lakini kwasababu natakiwa kutaja timu moja basi naipa City.
āChelsea hawatakuwa na Michuano yoyote ya Ulaya, hivyo itakuwa faida kwao, lakini inaweza kuchukua muda kidogo kuendana na kile anachowafundisha Conte.
āVivyo hivyo kwa Mourinho na Man Utd. Vilevile City na Guardiola- hivyo basi, labda kuna upenyo kwa Liverpool, Arsenal na Tottenham ā ambao wamekuwa na vikosi vyao vile vile pamoja na makocha wale wale.ā
GARY NEVILLE
- Man Utd 2. Arsenal 3. Man City 4. Liverpool
āUnited wana meneja na wachezaji wawili ambao wana ari kubwa ya ushindi. Uwepo wa Jose Mourinho, Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba ā na wachezaji wengine ambao walikuwepo awali, basi naiona United ikirejea kwenye uimara wake.
āKuna wachezaji ambao wanavaa tisheti za United na kuwaingia kwenye mioyo yao na kupambana kwa nguvu ā na hiyo sasa ndiyo Manchester United inavyopaswa kuwa.
āKwangu mimi, bingwa atakuwa Man Utd, Arsenal nafasi ya pili Arsenal, Manchester City nafasi ya tatu na Liverpool nafasi ya nne.
JAMIE CARRAGHER
- Man City 2. Chelsea 3. Man Utd 4. Liverpool
āKwa miaka mingi sana nimekuwa nikisema kwamba City wana kikosi bora, lakini hawafanyi kile kinachotakiwa na nadhani njaa ya mafanikio itarudi tena chini ya utawala wa Pep Guardiola.
āBila shaka, wanahitaji kusajili zaidi, lakini tayari wana wachezaji ambao wako vizuri tangu hapo awali kama David Silva, Sergio Aguero na Kevin De Bruyne. Hawa watatu watakuwa ni mwanga kwa wengine watakaokuja.
āKwa kuwa hawashiriki kwenye michuano yoyote ya Ulaya, nadhani Chelsea watafanya vizuri kwasababu watakuwa na muda mwingi wa kuzoeana mazoezini. Na tukumbuke kwamba ni miezi 12 tu imepita tangu wawe mabingwa, vilvile Antonio Conte ni kocha wa kiwango cha juu.
āNadhani Liverpool pia watanufaika kutokana na kutokuwa na Mashindano ya Ulaya.ā
Maoni