Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Paul Pogba:Manchester United wamnunua kiungo wa Ufaransa kwa £89m

MTEULE THE BEST

pogbaPogba amechezea timu ya taifa ya Ufaransa mechi 38

Paul Pogba: Manchester United wamnunua kiungo wa Ufaransa kwa £89m

Paul Pogba amesema huu "ndio wakati bora zaidi wa kurejea Old Trafford" baada yake kukamilisha kuhamia Manchester United kwa kununuliwa £89m kutoka Juventus, ambayo ni rekodi mpya ya dunia.
Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 23 amerejea miaka minne baada ya kuondoka United na kwenda Juventus kwa £1.5m mwaka 2012.
Pogba, ambaye ametia saini mkataba wa miaka mitano, ameongeza, "Hii ndiyo klabu bora kwangu kutimiza kila kitu ambacho kimekutumainia."
Meneja Jose Mourinho amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa huenda akawa nguzo ya klabu hiyo kwa mwongo mmoja ujao.
United watalipa mabingwa hao wa Italia euro 105m kumchukua Pogba, pamoja na nyongeza euro 5m (£4.5m) ambayo ni bonasi kwa kutegemea mafanikio yake pamoja na gharama nyingine.

Paul Pogba

Bei yake imezidi ya mshambuliaji wa Wales Gareth Bale aliyenunuliwa £85m kuhamia Real Madrid kutoka Spurs mwaka 2013.
Pogba alijiunga na United mara ya kwanza kutoka kwa klabu ya Le Havre ya Ufaransa mwaka 2009 akiwa na miaka 16, na akawachezea mechi chache kabla ya mkataba wake kumalizika Julai 2012.
Amecheza Juventus 178 na kuwafungia mabao 34 na kuwasaidia kufika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2015.
Klabu hiyo ya Serie A ilikuwa imeahidi kumpa mkataba mpya. Real Madrid nao pia walitaka kumnunua.

paul pogbaImage copyrightGETTY IMAGES

Wachezaji walionunuliwa ghali karibuni

  • 2013 - Gareth Bale £86m (Tottenham Hotspur hadi Real Madrid)
  • 2009 - Cristiano Ronaldo £80m (Manchester United hadi Real Madrid)
  • 2009 - Kaka £56m (AC Milan hadi Real Madrid)
  • 2001 - Zinedine Zidane £46m (Juventus hadi Real Madrid)
  • 2000 - Luis Figo £37m (Barcelona hadi Real Madrid)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...