Cristiano Ronaldo ambuliza Lionel Messi kwa pesa WANASOKA 10 WANAOLIPWA MKWANJA MREFU DUNIANI
MTEULE THE BEST
Kwa mujibu wa mtatndao wa sokkaa.com, wachezaji wawili bora duniani Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamewaacha wengine mbali katika kuvuta mkwanja mrefu kwa upande wa wacheza soka.
Ronaldo, ambaye hivi karibuni ameisaidia Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2026, anaongoza chat hiyo akiwa na mshahara wa £288,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi (sawa na kitita cha £15 million kwa mwaka) waka Messi akiwa nafasi ya pili kwa kulipwa vizuri anachukua kitita cha £275,000 (sawa na £14.5 million kwa mwaka).
Baada ya kukamilika kwa dili lililovinja rekodi ya uhamisho duniani la ada ya paundi milioni 89 (sawa na dola za Marekani milioni 115.98), Paul Pogba ambaye amesaini miaka mitano kuitumikia Manchester United mkataba wake unamfanya alipwe £290,000 kwa wiki.
1. Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Mshahara kwa wiki: £288,000 baada ya makato ya kodi
Mshahara kwa mwaka: £15 baada ya makato ya kodi
2. Lionel Messi (FC Barcelona)
Mshahara kwa wiki: £275,000 baada ya makato ya kodi
Mshahara kwa mwaka: £14.5 million baada ya makato ya kodi
3. Wayne Rooney (Manchester United)
Mshahara wa wiki: £260,000
Kwa mwaka anavuna mshahara: £13 million
4. Paul Pogba (Manchester United)
Mshahara wa wiki: £290,000 (kabla ya makato ya kodi)
Mshahara kwa mwaka:£13.9 million
5. Zlatan Ibrahimovic (Manchester United)
Mshahara wa wiki: £250,000
Kwa mwaka anaingiza: £11.4 million
6. Yaya Toure (Manchester City)
Mshahara wa wiki: £240,000
Mshahara wake kwa mwaka ni: £11.9 million
7. Sergio Aguero (Manchester City)
Mshahara wa kila wiki: £240,000
Mshahara wa mwaka: £11.9 million
8. Asamoah Gyan (Shanghai SIPG)
Mshahara wa kila wiki: £227,000
Mshahara wa mwaka: £11.8 million
9. Neymar (Barcelona)
Mshahara wa kila wiki: £220,000
Mshahara wa mwaka:£11.4 million
Mshahara wa kila wiki: £200,000
Mshara kwa mwaka: £10.9 million









Maoni