Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Brazil: Rais Lula kuchunguzwa kwa tuhuma za ufisadi

MTEULE THE BEST Image caption Lula ameongoza Brazili kuanzia 2003 mpaka 2011 Mahakama kuu nchini Brazil imesema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inácio Lula da Silva atachunguzwa ili kuthibitisha kama kweli alihusika katika kashfa ya ufisadi kwenye kampuni kubwa ya mafuta nchini humo Petrobras. Waendesha mashitaka nchini humo wamesema kuwa Lula alikuwa muhimili mkubwa katika utekelezwaji wa rushwa hiyo. Lula amekana kuhusika na kusema kuwa hizo ni mbinu za kisiasa za kumzuia kuwania urais mwaka 2018.

Udhibiti wa mipaka waanza Ulaya

MTEULE THE BEST Shirika jipya la kudhibiti mipaka na pwani la Umoja wa Ulaya limeanza shughuli zake katika mpaka baina ya Bulgaria na Uturuki, huku Umoja huo ukitarajia hatua hiyo itamaliza mzozo miongoni mwa wanachama. Maafisa wa Umoja wa Ulaya wamezindua mpango huo leo katika kivuko cha mpaka wa Andreevo ulioko baina ya Uturuki na Bulgaria ambao wahamijai wengi huutumia ili kuingia katika bara la Ulaya.  Lengo la kuanzishwa kwa kikosi hicho cha kudhibiti mipaka katika Umoja wa Ulaya ni kutafuta mfumo sawia utakao tumiwa kupambana na swala la uhamiaji haramu. Waziri wa mambo ya ndani wa Bulgaria  Rumyana Bachvarova  amesema kuwa uzinduzi huo wa leo ni jambo  muhimu kwa bara zima la Ulaya kuweza kutokea. Pia ameeleza kwamba kuzinduliwa kwa shirika hilo jipya ni mwanzo wa ushirikiano mzuri na hatua zitakazoleta mafanikio katika mipaka ya Ulaya. "Kuilinda mipaka yenye uhakika ndio jukumu letu kubwa hasa katika wakati huu wa mgogoro wa wakimbizi. Ili kufani...

Makubaliano ya Paris kuanza kutekelezwa 4 Novemba

MTEULE THE BEST Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi yataanza kutekelezwa kuanzia tarehe 4 Novemba.   Makubaliano hayo yataanza kutekelezwa siku 30 baada kuidhinishwa na zaidi ya nchi 55 zinazozalisha takribani zaidi ya asilimia 55 ya hewa chafuzi duniani. Juzi Jumatano Umoja wa Mataifa ulisema kuwa pande 73 za makubaliano hayo zinazozalisha asimilia 56.87 tayari zimeidhinisha makubaliano hayo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa taarifa iliyosema kuwa uungwaji mkono wa nguvu wa makubaliano hayo ya Paris kutoka kwenye jumuia ya kimataifa ni uthibitisho wa hitaji la haraka la uchukuaji hatua. Mataifa mawili yanayoongoza kwa uzalishaji wa hewa chafuzi duniani China na Marekani yaliidhinisha makubaliano hayo mwezi uliopita na kusababisha nchi nyingine saba wanachama wa Umoja wa Ulaya kuharakisha mchakato wao wa kuidhinisha makubaliano hayo. Makubaliano hayo yataanza kutekelezwa kabla ya kongamano...

BAKHRESA; apewa hekta elfu 10 na Rais MAGUFULI

MTEULE THE BEST Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amempa hekta elfu 10 mwenyekiti wa makampuni ya chakula ya Bakhresa ,kulima miwa na kuazisha kiwanda cha sukari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa wakwanza (kulia), Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega wakivuta kamba kwa pamoja kuashiria ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kusindika Matunda cha Bakhresa Mwandege mkoani Pwani Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amempa hekta elfu 10 mwenyekiti wa makampuni ya chakula ya Bakhresa ,kulima miwa na kuazisha kiwanda cha sukari ili kukidhi soko la sukari ya nyumbani na viwandani. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali serikali na menejimenti ya Bakhresa Group Akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa kampuni ya BAKHRESSA  FOOD PRODUCTS COMPANY baada ya kuzindua kiwanda cha kusindika...