Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Bomu la nyuklia la USSR lililoishangaza dunia

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha SPL Image caption Mfano wa bomu lililopewa jina Tsar Bomba Mapema asubuhi, mnamo 30 Oktoba 1961, ndege ya kuangusha mabomu ya Muungano wa Usovieti aina ya Tu-95 ilipaa kutoka uwanja wa kambi ya ndege za kivita ya Olenya katika rasi ya Kola kaskazini mwa Urusi. Tu-95 ilikuwa ndege kubwa sana yenye injini nne ambayo iliundwa mahsusi kubeba mabomu. Katika mwongo mmoja uliotangulia, Muungano wa Usovieti ulikuwa umepiga hatua sana katika utafiti kuhusu nyuklia. Marekani na USSR zilikuwa zimejipata upande mmoja wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia lakini baada ya vita, kukatokea Vita Baridi. Wasovieti baada ya kujipata wanakabiliwa na taifa pekee lililokuwa na silaha za nyuklia, iliona njia pekee ya kushindana vyema na Marekani ilikuwa ni kuwa na silaha zake za aina hiyo. Tarehe 29 Agosti 1949, Wasovieti walikuwa wamefanyia majaribio silaha yake ya kwanza ya nyuklia kwa jina 'Joe-1' katika eneo a...

Mji wa Tal Afar,Iraq wakombolewa

MTEULE THE BEST Image caption Tal Afar, Iraq Vikosi vya majeshi ya serikali ya Iraq vimefanikiwa kukomboa eneo zima karibu na mji wa Tal Afar kaskazini magharibi mwa Iraq ambapo kwa muda mrefu ilikuwa ni ngome ya wanamgambo wa kiislam, IS. Majeshi ya kawaida ya Iraq na wanamgambo wengi wa Shia ambao wanawasaidi wameelezea hali ilivyokuwa kwamba Vita kwa mji wa al-Ayadiya karibu na Tal Afar sasa imekwisha. Wanamgambo hao wa Islamic State wametoroka katika eneo hilo na kwenda kujihifadhi sehemu zingine baada ya kukimbia mji huo wa Tal Afar. Wanajeshi nchini Iraq wameelezea mapambano baina yao na wanamgambo wa IS kuwa yalikuwa makali kuliko ilivyokuwa katika mji wa Mosul.

Nyama ya Punda yasababisha 'bei kupanda' nchini Kenya

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Image caption Punda Shirika moja linalohusika na maslahi ya wanyama nchini Kenya, linasema bei ya Punda imepanda mara dufu nchini humo kwa sababu ya nyama ya mnyama huyo kuongezeka hasa katika taifa la china taifa ambalo hununua kwa wingi bidhaa ya mnyama huyo Kwa mujibu wa shirika hilo, sababu ya bei ya Punda kupanda kwa karibu asilimia 200 ni kutokana na ongezeka la biashara ya bidhaa za mnyama huyo huko Uchina ambako nyama ya punda ni kitoweo kilicho na walaji wengi. Awali kichinjio cha punda kimoja tu kilikuwa kimefunguliwa nchini Kenya kwa minajili ya kusindika nyama ya punda na kisha kuuzwa huko Uchina. Lakini sasa vichinjio vingine viwili vimefunguliwa kujaribu kukabiliana na mahitaji hayo yaliyoongezeka. Image caption Punda ni mnyama wa kubeba mizigo na kufanya kazi ya sulubu, lakini nyama yake sasa imekuwa kitoweo Mataifa kadhaa ya kiafrika yamepiga marufuku uuzaji ya nyama na bidhaa nyenginezo za punda, kwa aj...

Generali azungumzia kamatakamata ya viongozi wa upinzani

MTEULE THE BEST Sasa limekuwa ni jambo la kawaida la kila siku watu kushuhudia kiongozi wa upinzani akikamatwa na polisi kwa tuhuma za makosa yasiyokuwemo katika vitabu vya sheria nchini Tanzania. Ni jambo ambalo limeanza kuzoeleka kwamba wawakilishi wa wananchi – wabunge au madiwani –wanaweza kushikiliwa na vyombo vya usalama bila kujali kabisa wadhifa wao ndani ya jamii wala usahihi wa tuhuma zinazoelekezwa kwao, anasema Jenerali Ulimwengu. Katika shauri mojawapo, mbunge wa Arusha, Godbless Lema, aliwekwa mahabusu na kushikiliwa kwa muda wa miezi minne bila maelezo yo yote. Hatimaye alipewa dhamana na mahakama ya rufani ambayo iliwakaripia mahakimu wa mahakama za chini pamoja na mawakili wa upande wa mashitaka kwa kile ilichokiita ‘kunajisi sheria’ kwa kuwanyima watuhumiwa dhamana, ambayo ni haki yao ya msingi kabisa. Ingawaje Lema aliruhusiwa dhamana, amekuwa akilazimika kuhudhuria mahakama mara kwa mara kwa ajili ya kesi zinazomkabili ambazo zinahusu madai ya uchoc...

Mahujaji waanza ibada ya Hajji mjini Makka

MTEULE THE BEST Zaidi ya Mahujaji milioni mbili wa Kiislamu kutoka duniani kote leo Jumatano wanaanza ibada ya Hajji katika maeneo matakatifu ya Makka na Madina ikiwa ni nguzo kuu kwa kila muislamu kuitimiza katika maisha yake. Hii ni moja ya nguzo kuu za kidini ambayo kila Muislamu anapaswa kuitekeza angalau mara moja katika maisha yake ikiwa anao uwezo wa kufanya hivyo. Mwanzoni mwa Hajji leo, mahujaji walianza kwa kuzunguka nyumba ya mwenyezi Mungu ya Kaaba mjini Makka na kutekeleza ibada zinazoaminika kufuatilia nyayo za Mitume Ibrahim na Ismail. Zaidi ya mahujaji milioni mbili wanashiriki ibadi hii kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mamla za Saudia, idadi hii ikiwa ni zaidi ya waliohudhuria Hajji ya mwaka jana waliokadiriwa kufika milioni 1.8 na elfu 24,000 mwaka 1941. Afisa mmoja wa Indonesia ameliambia gazeti la Saudia kwamba jumla ya Mahujaji 221,000 kutoka Indonesia tayari wamefika mjini Makka ikiwa ndiyo idadi kubwa kutoka nje ya nchi. Mahujaji ...

Madaktari wapigana ndani ya chumba cha upasuaji, India

MTEULE THE BEST Image caption Madaktari wanaonekana wakitukanana kwa Kihindi Picha ya madaktari wawili wakipigana wakati walipokuwa wakimfanyia mgonjwa upasuaji, imesambaa katika mitandao ya kijamii Madaktari hao wawili wamesimamishwa kazi kwa muda nchini India, baada ya video kusambaa mitandaoni wakigombana vikali, huku wakiwa wamesimama kandokando ya mama mmoja mja mzito, wakati wa upasuaji. Taarifa kutoka Hospitali hiyo imethibitisha kuwa wawili hao wamesimamishwa kazi kwa muda. Video ya kisa hicho kilichotokea katika Hospitali ya Umaid iliyoko kaskazini mwa mji wa Rajasthan, imesambazwa pakubwa na kusababisha malalamishi makubwa. Afisa mmoja mkuu wa Hospitali hiyo ameiambia BBC kuwa, mwanamke aliyekuwa akifanyiwa upasuaji na mwanawe wako salama. Chanzo cha video hiyo bado haijabainika, lakini wakuu wamethibitisha kuwa kisa hicho kilifanyika hospitalini humo. Matusi mtandaoni Mara baada ya kuonekana kwa mkanda huo wa video mtandaoni, ripoti nyingi ilidai kuwa mwanam...