Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Zuma atakiwa kujibu mashtaka ya rushwa

MTEULE THE BEST Zuma atakiwa kujibu mashtaka ya rushwa Afrika Kusini Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imewasilishwa na Rais Jacob Zuma kupinga kufufuliwa kwa mashtaka ya ulaji rushwa dhidi yake. Bw Zuma na maafisa wengine wakuu serikali walikuwa wametuhumiwa kupokea mlungula wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, maboti ya kushika doria na silaha nyingine. Kuna jumla ya mashtaka 783 kuhusiana na mkataba huo wa mwaka 1999 wa ununuzi wa silaha za mamilioni ya dola. Zuma adaiwa kusinzia bungeni Jacob Zuma : Siogopi kufungwa jela Mashtaka hayo yaliwasilishwa mara ya kwanza dhidi ya Bw Zuma mwaka 2005 lakini yakaondolewa na waendesha mashtaka mwaka 2009 na kumuwezesha Bw Zuma kuwania urais. Hata hivyo, mwaka jana, Mahakama Kuu mjini Pretoria iliamua kwamba kiongozi huyo anafaa kujibu mashtaka hayo. Bw Zuma baadaye aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu ya Rufaa kupinga hatua ya kufufuliwa kwa mashtaka hayo. Rais huyo amekuwa akisisitiza kwamba ...

Sheikh Ponda ajisalimisha katika kituo cha polisi Tanzania

MTEULE THE BEST Image caption Sheikh Ponda wa Tanzania Katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa maeneo maalum mjini Dar es Salaam RPC Lazaro Mambosasa. Kiongozi huyo wa dini aliwasili katika kituo hicho cha polisi siku ya Ijumaa akiwa na wakili wake Abdallah Safari. Bwana Mambosasa siku ya Alhamisi alimwagiza Sheikh Ponda kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na matamshi ya uchochezi aliyotoa. MATANGAZO Sheikh Ponda apewa siku 3 kujisalimisha kwa polisi Tanzania Kulingana na kamanda huyo , Kiongozi huyo wa dini alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini na alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo akamatwa

Watu wawili wauawa maandamano ya Upinzani Kenya

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha AFP/GETTY Image caption Magari yaliyokuwa yamewabeba viongozi wa upinzani Nairobi yalirushiwa vitoa machozi Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya muungano wa upinzani katika mji wa Bondo, magharibi mwa Kenya. Taarisa zinasema wawili hao wamefariki baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji ambao inadaiwa walijaribu kuvamia kituo cha polisi cha Bondo katika kaunti ya Siaya. Mkuu wa polisi wa eneo hilo John Kiarie ameambia BBC kwamba hawezi kukanusha au kuthibitisha vifo hivyo kwani bado hajapokea maelezo ya kina kuhusu tukio hilo. Muungano wa upinzani National Super Alliance wake waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umekuwa ukifanya maandamano kushinikiza mageuzi kwenye Tume ya taifa ya Uchaguzi IEBC kabla ya uchaguzi mpya kufanyika. Raila Odinga ajiondoa kwenye uchaguzi Kenya Mgombea mwingine aruhusiwa kuwania urais Kenya Alhamisi, serikali ilipiga marufuku maandamano katika maeneo ya kati ya miji ya Na...

MAHAKAMA NA BUNGE KENYA ZATOA MAAMUZI MAGUMU

MTEULE THE BEST Mahakama, bunge Kenya zatoa maamuzi magumu uchaguzi wa Oktoba 26 Bunge la Kenya limepitisha marekebisho tata kuhusu sheria ya uchaguzi, likisema ikiwa mgombea mmoja atajitoa katika uchaguzi wa marudio mwingine atashinda moja kwa moja. Wapinzani wamekosoa na kususia kikao cha bunge. Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, alitangaza kujitoa katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26, akielezea wasiwasi kuhusu uadilifu na uwazi katika mchakato mzima. Sheria hiyo sasa inapaswa kutiwa saini na rais Uhuru Kenyatta. Hatua hiyo imekuja huku mahakama ya juu ikitoa hukumu kuwa mgombea aliepata chini ya asilimia moja ya kura katika uchaguzi wa Agosti 8 ambayo mahakama ya juu iliubatilisha, Ekuru Aukot ana haki ya kujumlishwa kwenye kura mpya. Jaji John Mativo alisema siku ya Jumatano kuwa hakuona sababu yoyote kwa Aukot kuzuwia kushiriki uchaguzi wa marudio. Aukot alipata karibu kura 27,000 kati ya zaidi ya kura milioni 15 zilizopigwa katika uchaguzi...

Trump: Muuaji wa Las Vegas ana matatizo ya kiakili

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Baadhi ya waliohudhuria tamasha hilo wakitoroka kufuatia shambulio la bwana Paddock Rais Donald Trump wa Marekani amemtaja muuaji wa watu 59 huku 527 wakijeruhiwa mjini Las Vegas kuwa mgonjwa aliye na akili punguani. Akizungumza katika ikulu ya Whitehouse , amesema kuwa ataziangazia upya sheria za umiliki wa bunduki katika siku za usoni lakini hakuelezea zaidi. Maafisa wa polisi wanajaribu kubaini kwa nini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa katika tamasha akiwa katika ghorofa ya 32 karibu na hoteli ya Mandalay Bay. Polisi walipata bunduki 23 katika chumba chake pamoja na vilipuzi. Kufikia sasa hakuna sababu mwafaka iliotolewa na wachunguzi hawajapata ishara zozote za shambulio hilo kuhusishwa na ugaidi wa kimataifa. Mshambuliaji aua watu 58 Las Vegas Marekani Polisi watafuta sababu ya mauaji Las Vegas Mauaji Las Vegas: Tunayoyafahamu kufikia sasa Kwa Picha: Mauaji Las Veg...

Viongozi wa Ulaya wakutana kuzungumzia 'mfumo wa dijitali'

MTEULE THE BEST Viongozi wa Ulaya wakutana kuzungumzia 'mfumo wa dijitali' Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Tallinn, Estonia, kuzungumzia "mfumo wa dijitali" licha ya kugubikwa na mjadala uliotokana na mapendekezo ya rais wa Ufaransa kuhusu mustakbali wa Umoja huo. Majadiliano yatakayoanza jioni ya leo (Septemba 29) yanatarajiwa kugubikwa na pendekezo la Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa la jinsi ya kutozwa ushuru makampuni makubwa makubwa ya kidijitali mfano wa Apple au Google, yanayotuhumiwa kutolipa ipasavyo kodi ya mapato. Ufaransa inapendelea kuona makampuni makubwa makubwa mfano wa Google au Apple yakitozwa ushuru unaostahiki badala ya mtindo unaotumika hivi sasa wa kutozwa katika nchi moja tu ya Umoja wa Ulaya, mfano wa Ireland au Luxemburg, kodi ya mapato kwa shughuli za kibiashara walizofanya katika nchi zote za Umoja wa Ulaya. Mada hiyo italeta malumbano katika mkutano huo wa kilele, ingawa haijaorodheshwa katika ajenda ya mazungu...

Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo September 30 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

MTEULE THE BEST Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo September 30  2017  kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa