Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Wafadhili waichangishia fedha Congo

Wafadhili wanakutana mjini Geneva Uswisi Ijumaa katika harakati za kuchangisha dola bilioni 1.7 kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo inakabiliwa na mzozo. Wataalam wanasema huenda mzozo huo ukapindukia na kuwa janga kubwa. Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na hofu kwamba  mizozo ya kikabila, ufisadi na hali mbaya ya usalama ni mambo yanayozusha hofu ya umwagikaji damu. Kwa wale walioachwa bila makao, kitisho ni cha kweli. Raia mmoja wa Congo alielezea mzozo wa kikabila katika mkoa wa Ituri kwa kusema, "ni kama wakati tulipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe." Kulingana na makadirio ya shirika la msalaba mwekundu karibu Wacongo 70,000 wamekimbilia Uganda kwa kuuvuka mto Albert tangu Januari. Ituri ni mkoa mmoja tu kati ya mingi ambayo makundi yaliyojihami na wahalifu wanawasumbua raia. Ukosefu wa usalama umezidisha idadi ya wakimbizi wa ndani ya nchi Zaidi ya hayo kuna mzozo wa kisiasa unaozunguka suala la urais ambapo watu wengi wanamtaka rais Joseph...

Waraka wa Papa kwa Wachile ni sawa na kutangaza 'hali ya hatari kiroho'

Waraka wa Papa kwa Wachile ni sawa na kutangaza 'hali ya hatari kiroho' Makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican yamesema hatua ya Papa Francis kuomba radhi kutokana na kashfa ya udhalilishaji wa kingono uliofanywa na padri na askofu Chile ni sawa na kutangaza hali ya hatari kiroho katika Kanisa la Chile.Papa amewaomba waathirika kwenda Rome ili awaombe radhi pamoja na kuwaita maaskofu wote wa Chile kwa mkutano wa dharura kujadili namna ya kurekebisha madhara yaliyotokana na kashfa hiyo ambayo imeichafua taswira ya Kanisa Katoliki nchini Chile na sifa ya Papa. Msemaji wa Vatican Grek Burke amesema waraka wa Papa kwa Kanisa Katoliki Chile ni kukiri kuwa alifanya makosa katika mtizamo kuhusu madhila waliyopitia waathiriwa. Hapo jana, Papa alikiri kuwa alifanya makosa makubwa katika maamuzi aliyoyachukua kuhusu sakata la udhalilishaji wa kingono Chile.

Mahakama Uganda yasikiliza kesi dhidi ya ukomo wa umri wa kuwania urais

Rais Yoweri Museveni ameongoza Uganda kwa ziadi ya miaka 30 Mahakama ya Kikatiba inasikiliza kesi iliyoletwa na upande wa upinzani kufuta marekebisho ya katiba ambayo yanatoa ukomo wa miaka ya kuwa rais. Wabunge waliipigia kura wa kishindo mwaka uliopita kufuta ukomo wa miaka 75. Ilimaanisha kuwa Rais Yoweri Museveni mwenye miaka 73, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30, anaweza kuwania tena mwaka 2021. Mawakili wa upinzani walitoa hoja kuwa marekebisho hayo yaliingizwa "kinyemela" hadi kuwa sheria, na bunge halikufuata kanuni zilizopaswa katika kuweka marekebisho hayo. Ulinzi umeimarishwa katika eneo la mahakama liliopo katika jiji la Mbale, mashariki mwa Uganda, na baadhi ya barabara zimefungwa kuepusha machafuko. Hii ni mara ya kwanza ombi la haki la kikatiba linasikilizwa , anaripoti mwandishi wa BBC Patience Atuhaire kutoka jiji kuu la Kampala. Miongoni mwa waomba haki ni wabunge wa upande wa upinzani,chama cha wanasheria Uganda na as...

KOCHA MBELGIJI: NIPENI TAIFA STARS NIIPELEKE KOMBE LA DUNIA 2022

BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kuanza mchakato wa kumsaka kocha mpya wa Taifa Stars, Mbelgiji, Adel Amrouche ameibuka na kufunguka kuwa, akipewa nafasi ya kuinoa timu hiyo, ataipambania ishiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar. Mbali na Kombe la Dunia, pia Mbelgiji huyo mwenye asili ya Algeria, amesema ataanza kwanza kupambana kuhakikisha Taifa Stars inashiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Cameroon. Hivi karibuni, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred, alisema mchakato huo wa kumsaka kocha, unaendelea vizuri ambapo wanaanza kupitia wasifu ‘CV’ mbalimbali za makocha walioomba nafasi hiyo baada ya kocha wa sasa, Salum Mayanga kumaliza mkataba wake tangu mwezi uliopita. Akizungumza na Championi Jumatatu , Kocha Amrouche aliyezaliwa Machi 7, 1968 katika Mji wa Kouba, Algiers nchini Algeria, amesema: “Nina uzoefu na soka la Afrika, nimefundisha timu ya taifa ya Kenya na Burundi, lakini pia kwenye kl...

Waangalizi huua Simba 250 kila mwaka nchini Tanzania

Afisa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) Dk. Dennis Ikanda alisema idadi ya simba ilianguka kutoka karibu 25,000 mwaka 2010 hadi 16,000 sasa.  Dodoma. Jumla ya viunga 250 huuawa kila mwaka nchini Tanzania na wachungaji wanaotisha hofu ya kutoweka kwa "mfalme wa jungle" katika nchi katika siku zijazo inayoonekana. Afisa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) Dk. Dennis Ikanda alisema idadi ya simba ilianguka kutoka karibu 25,000 mwaka 2010 hadi 16,000 sasa. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani Dr Ikanda alibainisha kuwa Tanzania bado inajiunga na idadi kubwa ya simba za nchi nyingine yoyote lakini ikiwa mwenendo wa poaching una wasiwasi. Mada ya Siku ya Wanyamapori ya Dunia ilikuwa "Panya Kubwa: Wadudu Wa Chini" na ilikuwa na lengo la kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kulinda paka kubwa. Kuhusu asilimia 80 ya simba huishi katika bustani za kitaifa, Dr Ikanda alibainisha, lakini ni asilimi...

CHADEMA YAIANDIKIA BARUA MAREKANI, UJERUMANI

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeziandikia barua Marekani na Ujerumani kuzitaka kuziangalia tuhuma zilizoelekezwa dhidi yao za kukihusisha na chama hicho katika kile kinachodaiwa kuwa ni mipango ya kuhatarisha usalama wa Tanzania. Barua mbili za Chadema ambazo zimeandikwa Machi mosi mwaka huu na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha chama hicho, Tumaini Makene, zimetaka balozi za nchi hizo nchini kujibu tuhuma hizo ambazo zilielekezwa na Cyprian Musiba aliyejitambulisha kama Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI. Gazeti hili ambalo limefanikiwa kuona barua hizo jana, Chadema kimesema kimeona umuhimu wa kuchukua hatua hiyo ili kupata mwitikio wa nchi hizo juu ya tuhuma hizo nzito ambazo zinatakiwa kuangaliwa zaidi. Katika barua yenye kumbukumbu No. C/HQ/ADM/KS/24/02  ambayo imeelekezwa kwa John Espinos ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi, Ubalozi wa Marekani, Chadema imeeleza kwamba Februari 25, mwaka huu mtu aliyejulikana kwa jina la Cyprian Musib...

Vladimir Putin asema Urusi ina kombora lisiloweza kuzuiwa

Haki miliki ya picha AFP Image caption Ilikuwa hotuba ya mwisho kwa Bw Putin kabla ya uchaguzi Urusi imeunda kombora jipya ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin. Bw Putin amekuwa akieleza sera zake muhimu za muhula wa nne, taifa hilo linapokaribia kufanya uchaguzi katika siku 17. Rais huyo anatarajiwa kushinda. Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale. Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo." Katika nusu ya kwanza ya hotuba hiyo yake kwa taifa, ameahidi kupunguza viwango vya umaskini nchini humo. Kisha, ameonesha mkusanyiko wa silaha mpya, likiwemo kombora alilosema linaweza "kufika pahala popote duniani". Hotuba hiyo ya Bw Putin imeendelea kw...