Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Merkel hajapata alichotarajia Washington

Kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel na  rais  wa  Marekani Donald Trump wameeleza tofauti zao kuhusiana  na  biashara na Jumuiya  ya  NATO  katika  mkutano  wao uliofanyika  katika Ikulu  ya White  House  ambako  walijaribu  kuonesha  hali  ya  uchangamfu licha  ya  hali  ya  wasi  swsi  baina  ya  washirika  hao  wawili. Angela Merkel akiingia Ikulu ya white House pamoja na rais Donald Trump wa Marekani Wakati  Trump anakaribia  kuweka ushuru  katika  biadhaa  za chuma na  bati  hivi  karibuni  ambavyo  vitaathiri mauzo  ya  nje  ya mataifa  ya  Ulaya, Merkel  amesema  uamuzi sasa  uko  mikononi mwa  Trump juu  ya  iwapo kutoa  msamaha kwa  mataifa  ya  Umoja wa  Ulaya. "Tulibadilish...

Kiongozi wa Korea Kaskazini avuka mpaka na kuingia Korea Kusini

Rais w a Korea kaskazini Kim jong un na mwenzake wa Kusini Moon Jae-in Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kuingia Korea Kusini kwa kuvuka mstari wa kijeshi uliowekwa kugawanya mataifa hayo mawili tangu vita vya Korea 1953. Katika hatua ilioshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina kiongozi wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa mikono katika mpaka huo. Bwana Kim alisema kuwa anatumai kwamba kutakuwa na mazungumzo ya kufana baada ya ufunguzi mzuri wakati mazungumzo hayo yalipoanza. Mkutano huo wa kihistoria utaangazia maswala ya silaha za kinyuklia na uwezekano wa makubaliano ya amani. Mengi yatakayozungumzwa ni mambo ambayo tayari yameafikiwa awali lakini wachanganuzi wengi bado wana wasiwasi kuhusu uaminifu wa Korea Kaskazini katika kukubalia kuacha shughuli ya utengezaji wa silaha za kinyuklia. Hatahivyo shughuli zote za taifa lote la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati y...

Uingereza yawatahadharisha raia wake wanaoelekea Tanzania Aprili 26

Bendera ya Uingereza Iwapo wewe ni raia wa Uingereza na unapanga kusafiri kuelekea Tanzania wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu ili kuhakikisha kuwa haujipati katika maandamano ya kisiasa yanayopangwa kufanyika tarehe 26 Aprili . Katika tahadhari ya usafiri iliotolewa na ubalozi wa Uingereza, wasafiri wameonywa kwamba ijapokuwa safari za kuelekea taifa hilo hazina matatizo yoyote, wageni wanaoingia nchini humo siku hiyo wanafaa kuwa makini kwani iwapo kutakuwa na maandano kunaweza kuwa na 'maafa'. Kulingana na gazeti la  The Citizen Tanzania , tahadhari hiyo ilitolewa kufuatia wito wa kufanyika kwa maandano dhidi ya serikali na mwanaharakati wa mtandaoni anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi. Anadai kwamba maandamano hayo ni ya kupinga ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na unyanyasaji wa haki za kibinaadamu. Barua ilioandikwa na ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari nchini Tanzania Serikali tayari imepinga madai hayo na kusema kuwa maandamano hayo yata...

Joshua Kimmich : Cristiano Ronaldo ni bora kuliko Leo Messi.

MTEULE THE BEST Cristiano Ronaldo Kabla ya kukabiliana na 'mashine ya lengo' ya Real Madrid Cristiano Ronaldo katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, Joshua Kimmich alisema kuwa kimataifa wa Kireno ni mchezaji kamili zaidi kuliko Leo Messi. Joshua Kimmich Joshua Kimmich anajitayarisha kwenda dhidi ya mchezaji wa "dunia kamili" katika Cristiano Ronaldowhen Bayern Munich akiwa na Real Madrid. Bayern inakaribisha wamiliki wa Ligi ya Mabingwa katika mechi ya kwanza ya Mechi ya kwanza ya Jumatatu, akitaka kulipiza kisasi kwa ukomeshaji wa msimu wa mwisho wa robo-mwisho. Ronaldo alifunga goli ya pili katika mguu wa pili wa tie hiyo na watalazimika kulipa kipaumbele tena, na nyota ya Ureno kwa fomu ya ajabu ya kufunga mara 15 katika michezo 10 ya Ligi ya Mabingwa msimu huu. Na mchezaji wa Bayern Kimmich anaamini kwamba mechi hiyo ya mabao ya malengo hufanya Ronaldo zaidi ya mchezaji "kamili" kuliko mpinzani wake wa Barcelona Lionel Messi. ...

Watu 10 wafa kwa kugongwa na gari kimakusudi nchini Canada

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema shambulio hilo ni baya na la kijinga, ni moja ya mashambulizi ya kutisha zaidi katika historia ya karibuni ya Kanada. Waziri Mkuu Trudeau ameonyesha huruma zake kwa wale wanaohusika na mkasa uliotokea. Amesema raia wote wanapaswa kujisikia wako salama kutembea katika miji na miongoni mwa jamii. Bwana Trudeau amesema hali hii inafuatiliwa kwa ukaribu, na kwamba Canada itaendelea kufanya kazi na vyombo vya usalama nchini kote kuhakikisha usalama wa wananchi wake. Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau Waziri wa usalama wa umma nchini Canada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili  tahadhari katika kiwango cha mashambulizi ya kigaidi. Waziri wa usalama wa umma nchini Kanada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili tah...

Korea Kusini na Kaskazini zajiandaa kwa mkutano wa kilele

Korea Kusini imesitisha matangazo ya propaganda kwenye eneo la mpaka na  Korea Kaskazini, kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kukutana kwa mazungumzo yanayotarajiwa kujikita juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.  Licha ya kuwepo matumaini ya Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa kinyuklia, Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa bado kuna njia ndefu ya kufikia suluhisho la mzozo wa Korea kaskazini  huku kiongozi huyo wa Marekani akijitayarisha kwa mkutano wa kihisitoria na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Korea zachukua hatua za maridhiano Kama sehemu ya ishara ya kujitayarisha kwa mazungumzo ya maridhiano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini ambayo ni ya tatu ya aina hiyo tangu kukamalizika vita vya Korea vilivyodumu kati ya mwaka 1950 hadi 1953, Korea Kusini imezima matangazo ya propaganda yanayotangazwa kupitia vipaza sauti katika eneo la mpakani. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Korea Kusini ilikuwa  ikitangaza hab...

Wanafunzi Tanzania wanavyopambana na unyanyasaji kwenye Usafiri

Modesta Joseph,mwanafunzi aliyeanzisha "Our cries" fursa inayompa mwanafunzi kushtaki anapokutana na unyanyasaji kwenye usafiri anapoenda shule Madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya walimu na wanafunzi katika shule za Nigeria huwa zinachukua vichwa vya habari vya magazeti mengi nchini humo lakini taarifa hizo huwa hazina muendelezo wowote wa hatua gani zimechukuliwa dhidi ya kesi hizi . Mwaka 2016,wasichana katika shule moja ya bweni mjini Lagos waliacha kufanya mtihani na kuandamana kupinga unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa mwalimu wa kiume. Jambo ambalo watu wote walivumilia tabia kama hizo miaka ya nyuma waliwaunga mkono. Mara nyingi wanafunzi wanakuwa hawapo kwenye nafasi ya kujitetea wanapokutana na wanyanyasaji kutokana na mila na desturi za kukaa kimya na kuheshimu waliokuzidi umri. Hali ambayo ni tofauti kwa binti mdogo kutoka Tanzania ,Modesta Joseph mwenye umri wa miaka 15 ambaye aliamua kutengeneza fursa kwa wanafunzi nchini mwake kutoa taarifa juu...