Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

       

CORONA| EPL, LIGUE 1, BUNDESLIGA, LALIGA, UEFA, UUROPA , ITALY, N.K ZASIMAMISHWA

Coronavirus : Mechi za Ligi ya soka ya England kuahirishwa hadi tarehe 3 Aprili Mechi za Ligi kuu ya soka ya England zitaahirishwa hadi tarehe 3 Aprili kufuatia baadhi ya wachezaji wa ligi hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona. Mashindano yote Ligi ya soka ya Ulaya, mkiwemo Championi Ligi na Ligi ya Ulaya, mechi ambazo zilitarajiwa kuchezwa wiki ijayo, zimeahirishwa kutokana na mlipuko wa coronavirus. Droo kwa ajili ya raundi ijayo, iliyopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, pia imeahirishwa. Katika Championi Ligi, mechi kati ya Manchester City dhidi ya Real Madrid, Juventus dhidi ya Lyon, Barcelona dhidi ya Napoli na Bayern Munich dhidi ya Chelsea zote zimeahirishwa. Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa. Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Machi pia zimesitishwa. Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatol...

PICHA| UZINDUZI WA KARAKANA YA KUU YA JESHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua karakana kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) - Lugalo jijini Dar es salaam. Machi 13, 2020

RAIS WA TANZANIA ATOA TAHADHARI KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORANA

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa tahadhari kuhusu ugonjwa unaotokana na virusi vya corona, akiwataka kutopuuza kwani mpaka sasa umegharimu maisha ya watu wengi duniani. Amezungumza na Umma wa Tanzania alipokuwa akizindua karakana ya jeshi hii leo jijini Dar Es Salaam. Katika kusisitiza tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa afya nchini humo, Ummy Mwalimu, Rais Magufuli amewataka raia kutopuuza tahadhari hizo. ''Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.'' ''Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua na hatua zimeanza kuchukuliwa waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua''. ''Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga...

Trump Kuchunguzwa na Bunge kwakutumia madaraka vibaya

Spika wa Bunge la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema Demokrasia ya Wamarekani iko mashakani, rais anawaacha bila chaguo Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi anasema bunge hilo litawasilisha mashtaka ya uchunguzi dhidi ya rais Donald Trump, kwa madai ya matumizi mabaya ya mamlaka yake. "Demokrasia yetu iko mashakani, rais anatuacha bila chaguo la kufanya," alisema kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Democrat. Ameyasema hayo siku moja baada ya kamati ya masuala ya sheria ya bunge kuanza kuangalia mashitaka yanayoweza kuwasilishwa dhidi ya rais huyo kutoka chama cha Republican. Bwana Trump aliwaambia Wademokrats kama watataka kumshitaki basi waharakishe. Alituma ujumbe wa Twitter muda mfupi kabla ya kauli za Bi Pelosi : " Kama mtanichunguza, mfanye sasa hivi, haraka, ili tuwe na kesi ya haki katika Seneti, ili nchi iweze kuendelea na shughuli za kawaida'': Mbunge wa Congres jimbo la California, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari A...

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 17.11.2019:

Gareth Bale Manchester United wanatarajia kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale,30, katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Sun on Sunday) Paris St-Germain wanawezekana kuwa kikwazo kikubwa kwa mpango wa Manchester United wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19 mwenye thamani ya pauni milioni 120. (Sunday Express) PSG pia wanamtaka kiungo wa Liverpool Adam Lallana,31.(Sunday Mirror) Manchester United wanamtazama kwa karibu winga wa West Bromwich Albion Matheus Preira, anayecheza kwa mkopo akitokea Sporting Lisbon. (Mirror) Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho Arsenal wanajiandaa kumuwania mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya taifa ya Uturuki, ambaye anaweza kuuzwa na Juventus kama ofa ya kuridhisha itatolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.(Tuttosport - in Italian) Barcelona wanajadili mkataba mpya na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32. (Mundo Deportivo - in Spanish) Mshambuli...

Maandamano ya kumuunga mkono Morales

Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika ubalozi wa Bolivia nchini Argentina wakimuunga mkono Evo Morales Mamia ya watu nchini  Argentina  wameandamana kuonyesha kumuunga mkono  Evo Morales   Rais wa  Bolivia  aliyelazimisha na jeshi la nchi hiyo kujiuzulu. Raia wa Bolivia wanaoishi nchini Argentina kwa uratibu wa asasi za kiraia zenye mrengo wa kushoto walikusanyika mbele ya ubalozi wa Bolivia nchini Argentina. Waandamanaji hao walilaani hila alizofanyiwa Rais Morales katika uchaguzi na baada ya uchaguzi na kutolea wito jamii la kimataifa kumuunga mkono Morales. Waandamanaji hao walibeba mabongo yenye ujumbe kama “Hatutaki mapinduzi Bolivia” pia walikuwa wakipeperusha bendera yenye rangi 7 inayowakilisha wakazi wa  eneo la milima ya Andes pamoja na bendera za Bolivia.