MTEULE THE BEST Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amemuita Rais Donald Trump kuwa ni "ni mtu asiyeweza kufikiri sawasawa" na kusema atalipa gharama kutokana na kauli zake za vitisho anazotoa dhidi ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema hii leo kuwa Trump ni mtu asiyestahili kuwa na hadhi ya kuwa na mamlaka aliyo nayo ya amiri jeshi mkuu wa nchi na kumuelezea Rais huyo wa Marekani kuwa ni mtu "mjanja na jambazi anayechezea moto". Matamshi hayo ya kiongozi wa Korea Kaskazini yanafuatia hotuba ya Rais Donald Trump aliyoitoa katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne wiki hii. Kim Jong Un amesema matamshi ya Trump yamemshawishi kuamini kuwa njia ambayo kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliyochagua kuifuata ni sahihi na kuwa ndiyo anapaswa kuifuata hadi mwisho na kuongeza kuwa alikuwa akifikiria kuchukua hatua kali. Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ameripotiwa akitishia nchi hiyo k...