Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mkutano wa Ujerumani na Uturuki kupunguza mivutano

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel atakuwa mwenyeji wa waziri mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglo kwa mazungumzo wakati nchi hizo mbili zikijaribu kumaliza mzozo wa tofauti zao. Mahusiano kati ya  washirika  hao  wa  jumuiya  ya  kujihami  ya NATO yamevurugika  kwa  kiasi  kikubwa , hususan  tangu  pale lilipofanyika  jaribio  lililoshindwa  la  mapinduzi  nchini  Uturuki mwaka  2016 na  kuanza  ukandamizaji  ambao ulishuhudia  mamia kwa maelfu  ya  watu  wakikamatwa, ikiwa  ni  pamoja  na Wajerumani  kadhaa  ama  wale  wenye uraia  pacha. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel Ujerumani  ambayo  ina  wakaazi  milioni tatu wenye  asili  ya Uturuki , mwaka  jana iliwashauri...

Urusi yaionya Marekani kutoingilia masuala ya Iran

Urusi imetoa onyo kwa Marekani kutojaribu kuingilia hali ya kisiasa nchini Iran. Urusi imetoa onyo kwa Marekani kutojaribu kuingilia hali ya kisiasa nchini Iran. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Ryabkov amekiambia kituo cha habari cha  TASS kuwa Urusi inaionya Marekani kutoingilia hali inayoendelea Iran. Kwa mujibu wa habari,Urusi inaamini kuwa hali ya Iran itarudi kuwa shwari. Urusi inaamini Marekani inajaribu kuingilia na kuharibu makubaliano ya JCPOA kati ya Iran na mataifa yenye nguvu katika suala zima la nyuklia. Hata hivyo Urusi imeahidi kusimamia na kulinda makubaliano hayo yaliyofanyika mwaka 2015. Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiandika maneno ya kuchochea maandamano nchini Iran kwa kupitia mtandao wake wa Twitter.

Nyota wa Tanzania kujenga kituo cha soka

Beki wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Baroka FC inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini , Abdi Banda amesema mwaka huu ana mpango wa kufungua kituo cha kukuza vipaji vya soka mkoani Tanga. " Malengo yangu ni kuwasaidia vijana wenzangu wa Kitanzania na mwaka huu natarajia kufungua kituo cha kukuza vipaji jijini Tanga," amesema Banda. Banda amesema atafanya hivyo kwasababu anatambua kuwa wapo vijana wengi ambao wana ndoto za kufika mbali zaidi kisoka , hivyo wanahitaji msaada kutoka kwa watu ambao wapo mbele katika soka . ''Unapocheza nje ya Tanzania ni vizuri kuonyesha mchango wako kwa vijana walio chini yako , kwahiyo hilo ndio lengo langu na sitaishia tu kujenga kituo nitaendelea kutoa vifaa vya michezo kwaajili ya vijana wenye ndoto za kuwa wachezaji wakubwa'' , ameongeza . Banda alisajiliwa na Baroka FC kwenye usajili wa k...

Liberia: George Weah amwalika Wenger sherehe ya kuapishwa kwake

MTEULE THE BEST George Weah alikuwa mchezaji Monaco Wenger alipokuwa meneja Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameambia BBC kwamba amepokea mwaliko kutoka kwa rais mteule wa Liberia George Weah kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwake baadaye mwezi huu. Wenger amesema: "Nimealikwa na George kwa siku hiyo ambapo ataapishwa kuwa Rais." Meneja huyo wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza Ligi Kuu ya Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja mchezaji huyo angekuwa rais. "Maisha ya jamaa huyu kwa kweli ni kama filamu. Ni ya kushangaza. Yanaweza kuunda filamu nzuri sana," amesema Wenger. "Nakumbuka nilipomuona mara ya kwanza Monaco alipofika na alikuwa anaonekana kukanganyikiwa kidogo, hakuwa anamjua mtu yeyote, na hakuwa anatazamwa na wengi kama mchezaji stadi na baadaye akaibuka na kuwa mchezaji bora duniani 1995 na leo hii sasa amekuwa rais wan chi. Ni kisa cha kushangaza," Wenger ameongeza. Wenger...

Tundu Lissu aitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati Tanzania

Mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema Bw Tundu Lissu amesema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali. Bw Lissu, akihutubia wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitalini, ameonekana kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwakandamiza wapinzani. Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali. Bw Lissu alikuwa akihutubu kutoka hospitali ya Nairobi jijini Nairobi ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa miezi minne sasa. Mbunge huyo wa Singida Mashariki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana. Bw Lissu amesema kufikia sasa anaamini hakuna uchunguzi wa maana kuhusu kushambuliwa kwake mnamo 7 Septemba unaendelea. Aidha, amesema Rais John Magufuli, ingawa aliandika ujumbe kwenye Twitter na pia kumtuma makamu wake Samia Suluhu Hassan, hajawahi...

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 05.01.2018

Ryan Sessegnon Kuna uwezekano mkubwa kwamba Liverpool watamruhusu Philippe Coutinho, 25, kuhamia Barcelona mwezi huu wa Januari kwa £140m. (Times) Chelsea wanamtaka meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone achukue nafasi ya Antonio Conte katika klabu hiyo mwisho wa msimu. (Times ) Chelsea wamezidisha juhudi zao za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Everton na England Ross Barkley, 24, na pia wameulizia kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa England na West Ham Andy Carroll, 28. (Mail) Mchezaji wa Celtic na Scotland Kieran Tierney, 20, amejumuishwa katika orodha ya mabeki wa kushoto ambao Manchester United wanawatafuta kuimarisha safu yao ya ulinzi, pamoja na kinda wa Fulham Ryan Sessegnon, 17. (Daily Record) Paris St Germain wanatarajiwa kutoa ushindani kwa Tottenham katika kutafuta saini ya Sessegnon ambaye thamani yake imekadiriwa kuwa £30m. (Mirror) Juventus wana imani kwamba watafanikiwa kumchukua Emre Can kutoka Liverpool bila kulipa ada yoyote mwisho...

Tunayoyafahamu kuhusu simu 'nyekundu na kijani' zilizotumika na nchi za Korea Kusini na Kaskazini

Hii ni simu inayounganisha Korea Kusini na Kaskazini katika nyumba ya uhuru Korea Kusini. Upande wa pili wa Korea Kaskazini ina simu kama hii Kila siku kwa miaka miwili, afisa wa Korea Kusini amechukua simu yenye rangi ya kijani na kumpigia afisa mwenzake upande wa pili , nje tu ya mpaka wa Korea Kaskazini. Lakini hamna aliyejibu simu hiyo. Hayo yote yakabadilika saa 9.30 ( 6.30 saa za GMT) tarehe 3 Januari 2018. Katika muda wa dakika 20,pande zote mbili walitumia laini zao wakiwa na matumaini ya kupungunza ugomvi baina ya nchi zao za Korea. Simu hiyo ipo katika kijiji cha mpaka wa Panmunjom, ambapo pamekuwa chanzo cha mawasiliano baina ya majirani hao ambao kimsingi bado wako vitani. Lakini tunafahamu nini kuhusu simu hiyo? 'Hamna Utani' Ni jambo linalokaa kama limetoka moja kwa moja katika nyakati za vita vya baridi - ni kweli. Likijengwa kwenye dawati mbalo ziliwekwa simu zenye rangi ya kijani na nyekunde pamoja na kompyuta, laini ya Kusini na Kaskazani ili...