Korea Kaskazini imesema huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia. Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni. Hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kusema imejitolea kuhakikisha silaha za nyuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea. Maandalizi ya mkutano huo wa Trump-Kim yamekuwa yakiendeleza, lakini sasa kumeingia shaka kuhusu hilo. Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limemnukuu naibu waziri wa mambo ya nje Kim Kye-gwan akisema iwapo Marekani "itatubana na kusisitiza kwamba ni lazima tusalimishe bila masharti silaha zetu za nyuklia basi hatutakuwa tena na hamu ya kushiriki mazungumzo hayo na itatulazimu kutafakari upya iwapo tutakubali mkutano unaotarajiwa kufanyika karibuni kati ya DPRK-US. Korea Kaskazini kir...