Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Rais wa Syria Bashar al- Assad kutembelea Korea Kaskazini

Kauli ya Assad imeripotiwa kutolewa a;ipokutana na Balozi mpya wa Korea Kaskazini nchini Syria Rais wa Syria, Bashar al-Assad anapanga kutembelea nchini Korea Kaskazini,Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeeleza. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuhodhi ziara ya Kiongozi wa nchi tangu alipoingia marakani mwaka 2011 Hivi karibuni amekuwa na shughuli nyingi za kidiplomasia, kukutana na Rais wa China mwezi Mei na anatarajiwa kuhudhuria mkutano na Donald Trump mwezi huu Syria, mshirika wa Korea Kaskazini, haijasema lolote kuhusu mpango huo unaoripotiwa. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishutumiwa kushirikiana katika mapngo wa kutumia silaha za kemikali.Lakini nchi hizi zimekana shutuma hizo Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa wazina vyombo vya Korea Kaskazini. Vilimnukuu bwana Assad siku ya Jumatano akisema ''ninakwenda kutembelea Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong-un." Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi...

Maafisa waliodaiwa kuhusika na ufisadi Kenya kupimwa na kifaa cha kuwafichua waongo

Uhuru Kenyatta ameahidi kukabiliana na ufisadi wakati alipochaguliwa kwa mara ya kwanza 2013 Maafisa wakuu wa serikali ya Kenya watalazimika kupimwa kwa kutumia kifaa cha kuwafichua watu waongo ikiwa ni miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi , rais Uhuru Kenyatta amesema. Bwana Kenyatta alisema kuwa kifaa hicho ambacho kitafichua maadili ya wafanyikazi ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo. Alikuwa akizungumza baada ya kufichuliwa kwamba shilingi dola bilioni 8 za Kenya zilipotea katika kitengo kimoja cha serikali. Takriban wafanyikazi 40 wa umma wanakabiliwa na mashtaka kufuatia kashfa hiyo. Kashfa hiyo ya ufisadi , ambayo ilifichuliwa na wauzaji bidhaa ambao walikuwa hawajalipwa , ilipelekea kuibiwa kwa fedha hizo katika shirika la vijana wa huduma kwa jamii NYS kupitia vyeti bandia na malipo ya ziada. Uchunguzi huo wa NYS -ukiwa mpango muhimu wa serikali ya rais Kenyatta kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana umeonekana ...

Washirika wa Marekani waungana kujibu vikwazo vya Trump

Nchi washirika wa Marekani zimekasirishwa na hatua za serikali ya Rais Donald Trump kuziwekea vikwazo vya kiushuru, vinavyolenga bidhaa za chuma cha pua na bati. Umoja wa Ulaya, Canada na Mexico, zimeapa kulipiza kisasi. Canada na Mexico zilitangaza mara moja hapo jana hatua za kujibu ushuru mpya uliowekwa na Marekani dhidi ya bidhaa zao za chuma cha pua na bati zinazoingizwa kwenye soko la nchi hiyo, nao Umoja wa Ulaya umesema tayari umejipanga kuujibu uamuzi huo wa serikali ya Trump. Waziri wa fedha wa Ujerumani Peter Altmeier amezungumzia uwezekani wa kushirikiana na Canada pamoja na Mexico, kuratibu mkakati wa pamoja dhidi ya Marekani. Tangazo hapo jana kutoka kwa waziri wa biashara wa Marekani Wilbur Ross la kuanzisha rasmi vikwazo vya kiushuru dhidi ya Umoja wa Ulaya, Canada na Mexico lilihitimisha kipindi cha miezi kadhaa ya sintofahamu, juu ya iwapo Marekani ingeelea kuziondoa nchi hizo kwenye orodha yake ya vikwazo vya kibiashara. Ulaya yakasirishwa Katika ...

Rais Magufuli afanya uteuzi tume ya madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Manya umeanza leo tarehe 01 Juni, 2018. Kabla ya uteuzi huo Prof. Manya alikuwa Kamishna wa Madini na alikuwa akikaimu nafasi ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. David Mulabwa kuwa Kamishna wa Madini. Kwa habari kamili soma hapa chini...

Vijana wavivu kufanyia kazi magereza

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samwel Opulukwa amesema Serikali itaanzisha Magereza katika wilaya hiyo ili kuwafunga vijana wavivu wasiotaka kufanya kazi. Mh. Opulukwa ameyasema hayo  wakati alipotembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo kilimo, afya na elimu inayotekelezwa na kampuni ya  Mgodi ya Shanta Mining katika kata ya Mbangala. Amesema vijana wengi katika kata hiyo hawapendi kufanya kazi licha ya kuwa na fursa nyingi ikiwemo ardhi yenye rutuba na badala yake wamekuwa wakijiingiza kwenye vitendo vya ulevi. Kiongozi huyo  wa wilaya amemweleza Kamishna Jenerali wa Magereza kuangalia uwezekano wa kujenga Gereza la Wilaya ili kuwafunga vijana ambao hawataki kufanya kazi pamoja na wahalifu wengine. “ Haiwezekani vijana mnashindwa kulima wakati Mashamba yapo,huku kwetu kuna fursa nyingi lakini mnashindwa kuzitumia, pale mkwajuni kulikua kuna kazi na mkandarasi lakini watu wakifanya kazi kidogo wakilipwa wanaingia mitini. Sasa tukiwa na gereza tutawafunga miezi...

Rwanda yapitisha sheria mpya kupambana na uhalifu wa mtandaoni

Bado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi. Bunge nchini Rwanda, Alhamisi lilipitisha sheria ya uhalifu wa mtandaoni yenye nia ya kuisaidia sekta za kiserikali na binafsi kudhibiti uhalifu huo. Bunge la juu lilipitisha muswada na kupeleka kwenye bunge dogo. Bado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi. Sheria inalenga kulinda taarifa za serikali na binafsi na miundombinu dhidi ya uhalifu wa mitandaoni na mashambulizi ya mitandaoni, kwa mujibu wa Wizara ya habari na mawasiliano na Teknolojia ya Rwanda. ''kwa sasa tunashuhudia mashambulizi ya mitandaoni duniani kote. Mashambulizi ambayo yanatishia usalama wa uchumi na usalama wa taifa,'' alieleza Agnes Mukazibera, Rais wa Bunge la Rwanda, baada ya kura. Sheria itaisaidia serikali kufanya uchunguzi vitisho vyovyote na kushtaki dhidi ya vitendo hivyo katika taasisi binafsi na za umma na kuitetea nchi dhidi ya...

Mgogoro wa Uingereza na Urusi waikwamisha Chelsea

Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich, amesitisha upanuzi wa uwanja wa Stamford bridge unaomilikiwa na klabu hiyo kutokana na nchi hiyo kushindwa kushughulikia kibali chake cha kuishi nchini humo. Abramovich tayari alikuwa ameshaweka mezani kiasi cha Paundi bilioni 1, kwaajili ya utekelezaji wa mpango huo, lakini amesimamisha ujenzi usianze hadi atakapojua hatima ya kibali chake cha kuishi. BBC wameripoti kuwa Visa ya Roman Abramovich ambaye ni raia wa Urusi, imekwisha muda wake ndani ya wiki kadhaa sasa, lakini amekuwa akicheleweshwa kupatiwa kibali kutokana na mvutano wa kidipromasia kati ya Uingereza na Urusi. Roman mwenyewe amesisitiza kuwa hawezi kuwekeza kwenye nchi ambayo hana kibali cha kuishi huku akieleza kuwa kitendo hicho hakiingiliani na shughuli zingine za uendeshaji wa klabu hiyo. Tukio la kupewa sumu kwa jasusi wa zamani wa Urusi aliyekuwa nchini Uingereza Sergei Skripal, mapema mwaka huu, ndio limeelezwa kuwa chanzo cha ushirikiano mdogo kati ya nchi hiz...