Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Raia wajitokeza kumshinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe

Maelfu ya raia wa Zimbabwe wamejitokeza barabarni hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go. Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40. Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala. Kikubwa kinachozozaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka. Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina. MUgabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka. Zaidi ya hayo Bw. Mugabe angependa kuendelea kuwa u...

Pentagon yamtaka Trump kujiuzulu kimakosa Ndio idara inayosimamia nambari za siri makombora, Idara inayosimamia usalama wa Marekani na mkuu wake ni rais wa Marekani ambaye hupendelea sana kutumia mtandao wa Twitter

Pentagon yamtaka Trump kujiuzulu kimakosa Ndio idara inayosimamia nambari za siri makombora, Idara inayosimamia usalama wa Marekani na mkuu wake ni rais wa Marekani ambaye hupendelea sana kutumia mtandao wa Twitter Ujumbe huo ambao pia uliwataka wanasiasa wengine wawili wa Marekani kujiuzulu kufuatia madai ya unyanyasaji wa kijinsia ulitumwa kutoka kwa akaunti ya @ProudResister Ndio idara inayosimamia nambari za siri makombora, Idara inayosimamia usalama wa Marekani na mkuu wake ni rais wa Marekani ambaye hupendelea sana kutumia mtandao wa Twitter. Lakini inapofikia wakati wa kusimamia akaunti yake ya mtandao huo, the Pentagon inafaa kuimarisha uwezo wake. Siku ya Alhamisi idara hiyo ya ulinzi ilituma ujumbe kimakosa katika mtandao wake wa Twitter ukimtaka rais Trump kujiuzulu. Ujumbe huo ambao pia uliwataka wanasiasa wengine wawili wa Marekani kujiuzulu kufuatia madai ya unyanyasaji wa kijinsia ulitumwa kutoka kwa akaunti ya @ProudResister, mwanaharakti ambaye ni mkosaji mkuu wa...

Pogba na Ibrahimovic kucheza dhidi ya Newcastle Jumamosi

Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wataorodheshwa katika kikosi cha Manchester United katika mechi ya Jumamosi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford Zlatan Ibrahimovic na Zlatan Ibrahimovic Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wataorodheshwa katika kikosi cha Manchester United katika mechi ya Jumamosi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford. Mshambuliaji Ibrahimovic , 36, bado hajashirikishwa katika mechi yoyote msimu huu baada ya kupata jeraha la goti mnamo mwezi Aprili. Kiungo wa kati Paul Pogba , 24, hajaichezea timu yake tangu alipopata jeraha la nyuma ya goti dhidi ya klabu ya Basel mnamo mwezi Septemba. Beki Marcos Rojo pia anapatikana na mkufunzi Jose Mourinho alisema kuwa wote wataorodheshwa. ''Paul unaweza kuona. Unaweza kugundua kwamba kulikuwa na Manchester United msimu huu kabla na hata baada ya jeraha lake'', aliongezea Mourinho. ''Ana uwezo ambao hubadilisha vile tutakavyocheza mechi z...

HECHE AMSHUKURU SPIKA KWA KUMLINDA ASIKAMATWE

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amekiri bila busara za Spika wa Bunge kutumika leo angekuwa amekamatwa leo na polisi wamedaiwa kutoka Morogoro waliokuwa eneo la Bunge kwa nia ya kumkamata. Mh. Heche amweka hilo wazi jioni hii huku akikosoa matumizi mabaya ya rasilimali iliyotumiwa. "Nimepokea barua ya polisi asubuhi leo wakinitaka kuripoti Morogoro eti kwa kosa la kumsindikiza na kufanya mkutano jimboni kwa Mh Lijualikali alipotoka gerezani mwezi wa 4" Amesema Heche na kuongeza; "Kabla hata ya kuitikia wanataka kunikamata bila busara za spika wangenikata. Matumizi mabovu ya rasilimali" Kabla ya taarifa hii kutoka Mapema leo Heche alikiri kupokea wito unaomtaka kwenda kuhojiwa Morogoro. "Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.

Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza

Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano. Alihudhuria sherehe za kufuzu kwenye mji mkuu Harare. Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi. Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo. Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza. Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais.

HISTORIA YA MAISHA YANGU NILIPOKUWA URUSI KAMA NILIVYOSIMULIA NIKIWA GLOBAL PUBLISHERS,SEHEMU YA 1

MJUE DR. LOUIS SHIKA HISTORIA YA MAISHA YANGU NILIPOKUWA URUSI KAMA NILIVYOSIMULIA NIKIWA GLOBAL PUBLISHERS,SEHEMU YA 1 Dkt. Louis Shika ambaye amepata umaarufu mkubwa baada ya kushiriki katika mnada wa nyumba za Said Lugumi jijini Dar es Salaam na baadaye ‘kukwaruzana’ na jeshi la polisi kutokana na mchakato wa mnada huo, amefunguka engi kuhusu maisha yake. Katika simulizi hiyo, Dkt Shika ambaye hivi sasa ni maarufu kama ‘900 Itapendeza’ kutokana na mambo yaliyojiri katika mnada huo, alianza kwa kusema kwamba neno ‘daktari’ linalotangulia jina lake ni la kitaalam, yaani kweli yeye ni daktari wa binadamu akiwa alisomea taaluma hiyo nchini Urusi. “Nilisomea utaalam huo nchini Urusi nilikokwenda mwaka 1984 kwenda kuchukua digrii ya kwanza ya miaka saba ambayo niliimaliza mwaka 1991,” anasema daktari huyo mwenye mwili wa kiasi na kimo kirefu. Anaendelea kusema kwamba mwaka huohuo aliamua kuunganisha masomo apate digrii ya pili ya mag...

Mamba' ambaye amegeuka kumuuma Mugabe

Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.   Mnangagwa amekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kumrithi Mugabe Imekuwa siri ya wazi nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kuwa Emmerson Mnangagwa angechukua nafasi ya Robert Mugabe na kuwa rais. Lakini Bwana Mugabe alionekana kucheza na hisia zake- wakati mwingine akimpandisha cheo ndani ya chama tawala cha Zanu- PF na serikalini na kuongeza tetesi ya yeye kuwa mrithi mtarajiwa lakini baadaye alishushwa cheo baada ya Mnangagwa kuonekana kuonesha nia zake mapema mno. Baada ya kutenguliwa, imeonekana kama subira ya mwanaume huyo maarufu kama "mamba" hatimaye imeisha. Baada ya Rais Mugabe kumtengua na kumshutumu kwa mfisadi, wafuasi wake na vikosi vya usalama waliingilia kati kwa niaba yake. Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa Mnangagwa ...