Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Wabunge 19 Chadema kulinda kura Dodoma

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamesema watawatumia wabunge kumi na tisa wa chama hicho kulinda kura katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kizota katika jiji la Dodoma.  Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea). Viongozi walitoa kauli hiyo jana nje ya ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota muda mfupi baada ya mgombea udiwani kata hiyo kupitia Chadema, Omar Bangababo kurejesha fomu ya ugombea kata hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, Iddy Kizota amesema watawatumia wabunge wa Chadema kulinda kura za mgombea kutokana na kuwapo kwa hujuma za kuwapiga mawakala na kuwaondoa vituoni kwa lengo la kubadilisha matokeo. Hata hivyo Kizota amesema kulikuwepo na njama kubwa ambazo zilikuwa zikifanywa na Ofisi Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu kwa kutaka kumkwamisha mgombea wa Chadema kwa kumwekea vikwazo visivyokuwa na sababu. “Unaweza kujiuliza msimamizi wa uchaguzi ...

Serikali Uganda yaondoa mashtaka ya uhaini dhidi ya Bobi Wine

Wine alifikishwa katika mahakama ya jeshi mjini Gulu ambapo maamuzi hayo yalitolewa baada ya serikali kumshtaki kwa kumiliki bunduki kinyume cha sheria - Kuachiliwa huru kwake kwa muda kuliwadia baada ya shinikizo tele kutoka kwa raia na hali tete kuendelea kushuhudiwa nchini Uganda - Wine alikamatwa tena mara baada ya kuachiliwa huru na kuwasilishwa katika mahakama ya raia na sasa ataendelea kuiziliwa hadi Agosti 30, 2028 Serikali nchini Uganda imeondoa mashtaka ya uhaini dhidi ya Mbunge wa Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyi, almaarufu Bobi Wine, kufuatia hali tete na ghasia zilizoshuhudiwa nchini humo kutoka kwa raia waliotaka aachiliwe huru. Wine, ambaye amekuwa kizuizini kwa muda wa wiki moja sasa, alipewa uhuru huo wa muda katika mahakama ya jeshi mjini Gulu, Alhamisi, Agosti 23, na kukamatwa tena. Maandamano yamekuwa yakishuhudiwa maeneo mbalimbali nchini Uganda na pia Kenya yakilenga kuishinikiza serikali ya Uganda kumwachilia huru Bobi Wine. Picha: NTV...

Rais wa Tanzania afiwa na dada yake

Rais Magufuli alipoenda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Dada yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. Hapo jana Rais Magufuli alienda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika hospital hiyo ya Bugando na rais alisema kwamba hali ya dada yake sio nzuri. Bi.Monica Magufuli alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 (alizaliwa tarehe 25 Novemba, 1955) na ameacha watoto 9 na wajukuu 25

TETESI ZA SOKA ULAYA HII LEO

mteulethebest Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Christian Eriksen Paris St-Germain wanaandaa pauni milioni 100 kwa ofa ya mchezaji wa Tottenham mwenye miaka 26 raia wa Denmark Christian Eriksen. (Express) Schalke wana nia ya kumasaini mchezaji mwenye miaka 22 raia wa England Reuben Loftus-Cheek kwa mkopo lakini Chelsea haunda wasiruhusu kuondoka kwake. (Telegraph) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Matteo Darmian Beki wa Manchester United Matteo Darmian anataka kuondoka Old Trafford na Juventus, Napoli na Internazionale wanamwinda mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Italia. (Manchester Evening News) Meneja wa Manchester United Jose Mourinho aliachanganyikiwa kufuatia madai ya Paul Pogba ya kuwepo uhusiano mbaya kati yao siku ya Ijumaa. (Telegraph) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Marcus Bettinelli Kipa Marcus Bettinelli, 26, anaweza akaamua kuondoka Fulham baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya kwanza ya msimu. (Mail)...

Luis Enrique kocha mpya wa Uhispania

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameteliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania Kocha  wa  zamani  wa  klabu  ya  Barcelona  Luis Enrique ametia saini mkataba  wa  miaka  miwili  kuchukua  hatamu za kuifunza  timu ya  taifa  ya  Uhispania. Anachukua  nafasi  ya  Julen lopetegui, ambaye  alifutwa  kazi katika  mkesha  wa  kuanza  kwa  fainali  za kombe  la  dunia  baada  ya  kukubali kazi katika  timu  ya  Real Madrid. Fernando Hierro alichukua  udhibiti wa  timu  hiyo  kwa  muda  kwa ajili  ya  fainali  hizo, ambapo  mabingwa  hao  wa  mwaka  2010 wa kombe  la  dunia  waliondolewa  katika  awamu  ya  mtoano na wenyeji Urusi

Maoni: Malumbano ya Brexit yazidi London

Kama Uingereza itashindwa kufafanua kuhusu ni nani anayeongoza utaratibu na kutoa maamuzi muhimu kuhusu Brexit, Umoja wa Ulaya utalazimika kuendelea kusubiri tu. Kwanza, Waziri anayehusika na masuala ya Brexit David Davis alijiuzulu, kisha Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni na aliyeongoza kampeni za kuitaka Uingereza kujiondoa Ulaya Boris Johnson akafuata. Wanalivuruga jaribio la Waziri Mkuu Theresa May la kuishawishi serikali yake kukubali Uingereza kuendeleza mahusiano ya karibu na Umoja wa Ulaya baada ya Brexit. Kujiuzulu huko kulikoratibiwa kwa mawaziri hao wenye misimamo mikali kuhusu Brexit kunaitumbukiza serikali ya May katika mgogoro na kuvuruga matumaini ya Umoja wa Ulaya ya kuweza hatimaye kuanza, katika wiki chache zijazo, mazungumzo muhimu kuhusu makubaliano ya kutengana na mahusiano ya usoni kati ya Uingereza na umoja huo. Ni Ijumaa iliyopita tu ambapo May alijaribu, kulazimisha kuliunganisha baraza lake la mawaziri linalozozana. Lakini kama mambo yanavyokwend...