Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail.
Hii
ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kwamba kati ya pesa
anazokusanya kupitia wakfu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia
moja zinazotumiwa kufaa jamii.Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika.
Drogba, 38, ametoa taarifa akisema habari hizo ni za “uongo na za kumharibia sifa
Tume inayodhibiti mashirika ya kusaidia jamii yaliyosajiliwa Uingereza imesema inachunguza “madai ya ukiukaji wa sheria”.
Kwenye taarifa yake, Drogba amesema: “Hakuna ulaghai, hakuna ufisadi na hakuna udanganyifu.”
Drogba, raia wa Ivory Coast, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Canada kwa sasa amewatuhumu wanahabari wa Daily Mail kwa kuweka hatarini maisha ya maelfu ya watoto wa Afrika.
Maoni