Rais Magufuli ametoa onyo kali
kwa
wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze
kwa bei kubwa.
Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya
pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko
Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na
ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati
akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani
Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo,
anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.
Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza
kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu
wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari
wako katika mchakato wa kuagiza makontena ya
sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara
walioficha bidhaa hiyo.
Maoni