MTEULE THE BEST
Japan imepeleka mtambo wa kutibua makombora magharibi mwa taifa hilo kufuatia tishio la Korea Kaskazini kwamba itarusha kombora la masafa marefu katika kisiwa cha Guam nchini Marekani.
Mtambo huo kwa Jina PAC3 (Patriot Advanced Capability-3) umepelekwa katika eneo la shimane, Hiroshima na Kochi ambapo Pyongyang inasema kombora lake litapaa kabla ya kuanguka katika maji ya Guam.
Jeshi la kulinda baharini la Japan limeripotiwa kutuma mtambo wa kutibua makombora katika bahari ya Japan likiwa na mfumo wa kufuatilia makombora ya masafa marefu
Maoni