Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Usain Bolt aumia na kushindwa mbio zake za mwisho mashindano ya dunia ya IAAF

MTEULE THE BEST

Usain BoltHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUsain Bolt ameshinda dhahabu 11 mashindano ya ubingwa wa dunia

Usain Bolt aliumia na kushindwa kumaliza mbio zake za mwisho za ubingwa wa dunia jijini London, na mwanariadha mwenzake Yohan Blake anasema huenda kucheleweshwa kwa mbio hizo kulimwathiri.
Bolt alipata mkakamao wa misuli na kulazimika kuondoka uwanjani alipokuwa akikimbia mbio za kupokezana vijiti za 4x100m ambazo timu ya Uingereza ilishinda.
Yohan Blake alisema hilo: "Mbio zilicheleweshwa dakika 10, tuliwekwa tukisubiri kwa dakika 40. Ilitushangaza sana.
"Watuweka muda mrefu sana tukisubiri."
Bolt alikuwa ametumai kwamba angemaliza maisha yake ya ukimbiaji kwa kushinda dhahabu mbili mashindano hayo ya London lakini ameondoka sasa na nishani ya shaba pekee aliyoishinda kwenye mbio za mita 100 wikendi iliyopita.
Sekunde chache baada yake kupokezwa kijiti awamu ya mwisho ya mbio hizo, alitatizima na kuanguka sakafuni.
Daktari wa timu ya Jamaica Kevin Jones amethibitisha kwamba Bolt alipatwa na mkakamao wa misuli ya mguu wake wa kushoto.
"Ilikuwa dakika 40 na walitoa nishani kwa washindi wa mbio mbili kabla yetu kukimbia," aliongeza bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 Blake.
"Tulikaa tukipasha misuli joto na kusubiri, kisha tunapasha misuli moto tena na kusubiri. Nadhani hilo lilitwathiri.
"Inauma kumuona jagina halisi, bingwa halisi akiingia uwanjani na kutatizika kwa namna hiyo."
Bingwa wa mbio za 110m za kuruka viunzi Omar McLeod, aliyeongoza timu ya Jamaica ambayo ilikuwa imeshinda ubingwa wa mbio za 4x100m katika makala manne yaliyopita ya ubingwa wa dunia, alikubaliana na mtazamo wa Blake.

Usain BoltHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Sherehe za kumuaga Mo Farah baada yake kumaliza nafasi ya pili mbio za 5000m zilionekana kuchelewesha ratiba, na pia Farah alikabidhiwa nishani yake kabla ya fainali ya mbio hizo za kupokezana vijiti.
"Inauma sana. Nilijitolea kabisa na nilitaka sana kumuona Usain akiondoka kwa ushindi, au hata kama ingekuwa nishani tu. Inashangaza bwana, tulisubiri muda mrefu. Nilikunywa chupa mbili za maji.
"Lakini jina la Usain Bolt litasalia kukumbukwa."
Mshindi wa mbio za 100m Justin Gatlin alisema Bolt 'ndiye bado bora zaidi duniani' baada yake kushinda nishani ya fedha na timu yake ya Marekani.

Usain BoltHaki miliki ya pichaEPA
Image captionUsain Bolt alikosa kushinda dhahabu mashindano ya ubingwa wa dunia mara ya mwisho 2007

Alikiri kwamba huenda hali ya hewa ilimwathiri Bolt.
"Nafikiri ni hali ya hewa iliyomsababishia Bolt jeraha. Lakini bado ndiye bora zaidi duniani. Huu ni wakati wa kuaga, naanza kumkosa tayari. Sehemu ya kupashia misuli moto, huwa tunaheshimiana na tulisalimiana. Usain Bolt ni mwanariadha mzuri sana."

Usain BoltHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionBolt (wa nne kutoka kulia) alipokuwa anaumia

Nishani alizoshinda Usain Bolt
2007 Ubingwa wa DuniaFedha (200m), Fedha (4x100m kupokezana vijiti)
2008 OlimpikiDhahabu (100m), Dhahabu (200m)
2009 Ubingwa wa DuniaDhahabu (100m), Dhahabu (200m), Dhahabu (4x100m kupokezana vijiti)
2011 Ubingwa wa DuniaDhahabu (200m), Dhahabu (4x100m relay)
2012 OlimpikiDhahabu (100m), Dhahabu (200m), Dhahabu (4x100m kupokezana vijiti)
2013 Ubingwa wa DuniaDhahabu (100m), Dhahabu (200m), Dhahabu (4x100m kupokezana vijiti)
2015 Ubingwa wa DuniaDhahabu (100m), Dhahabu (200m), Dhahabu (4x100m kupokezana vijiti)
2016 OlimpikiDhahabu (100m), Dhahabu (200m), Dhahabu (4x100m kupokezana vijiti)
2017 Ubingwa wa DuniaShaba (100m)

Mada zinazohusiana

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...