MTEULE THE BEST
Zaidi ya manyatta 100 za jamii ya Maasai zinadaiwa kuchomwa moto na mamlaka za mbuga ya wanyama pori karibu na mbuga ya wanyama pori ya Serenegeti.
Mamia wa watu wanaripotiwa kubaki bila makao kutokana na kuondolewa kwa jamii hii ya wafugaji.
Kijana mmoja wa kimasai anaripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.
Hii ni sehemu ya mzozo wa muda mrefu kati ya jamii ya Maasai na mamlaka ambazo huendesha shughuli za uwindaji kwa watalii.
Serikali ya Tanzania ina mipango ya kubuni eneo la ukubwa wa kilomita 1500 mraba kwenye mbuga hiyo, kwa kampuni yenye makao yake nchini Dubai ambayo hutoa huduma za uwindaji kwa watalii matajiri kutoka Milki ya nchi za kiarabu.
Mipango hiyo itasababisha watu 30,000 kupoteza makao na matatizo mengine kwa jamii ya Masai ambayo hutegemea malisho kwa mifugo wao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwani Kerry Dukunyi ameambia BBC kuwa wanavijiji wamepoteza mali katika kisa hiki cha hivi punde.
"Kiwango kikubwa cha chakula chetu kimeharibiwa.Tumepoteza chakula kingi," alisema
"Mifugo kadhaa pia hawajulikani waliko."
Maoni