Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Kisanduku cha ndege ya EgypAir chapatikana

MTEULE THE BEST   Kikosi cha Misri kilichokuwa kikitafuta mabaki ya ile ndege ya Egypt-Air iliyoanguka katika bahari ya Mediterranea, kinasema kimepata kisanduku cheusi cha kuhifadhi mawasiliano ya ndege. Watafutaji hao wanasema kuwa, kifaa hicho kilikuwa kimeharibika, pale walipokipata chini ya sakafu ya bahari. Mawasiliano ya ishara ya kifaa hicho yalinaswa na meli moja ya kijeshi ya Ufaransa, majuma mawili yaliyopita. Ndege hiyo ya EgyptAir chapa 804 muundo wa Airbus 320 na iliyokuwa ikitokea Paris, Ufaransa kuelekea Cairo, Misri, ilianguka na kuwauwa abiria wote 56 na wahudumu 10 waliokuwa ndani yake.

Wasomali 18 wafa ndani ya bohari nchini DRC

MTEULE THE BEST   P olisi nchini Zambia, wanasema kuwa wahamiaji 18 wenye asili ya Kisomali, wamefariki walipokuwa wakipelekwa kwa njia haramu kuingia katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Walikuwa wamebebwa ndani ya bohari lililokuwa na mzigo wa Samaki. Kamishina mmoja mkuu wa polisi nchini Zambia Hudson Namachila, amesema kuwa lori hilo lilisimama ndani ya mpaka wa Kongo pale baadhi ya wahamiaji haramu waliokuwa wameishiwa na hewa, walipoanza kugonga gonga bohari hilo wakiwa ndani, kuwaashiria madereva wawafungulie ambao walikuwa wamekamatwa. 11 kati ya wasomali hao 44 tayari walipatikana kuwa wamekufa huku wengine saba wakifariki baadaye. 27 walionusurika kufa wametiwa mbaroni.

Vikosi viliwaua zaidi ya watu 400 Ethiopia

MTEULE THE BEST   V ikosi vya usalama nchini Ethiopia vimewaua zaidi ya watu 400 wakati wa maandamano ya hivi majuzi ya kupinga serikali. Shirika la haki za binadamu lenye makoa yake nchini Marekani HRW, kwenye ripoti ya maandamano ya jamii ya Oromo ,limetoa orodha ya majina ya zaidi ya watu 300 linalosema waliuawa. Serikali imethibitisha kuwa waandamanaji walikufa, lakini pia imesema kuwa HRW haikusema ukweli kuhusu idadi. Maandamano hayo yalianza kutokana na hofu kuwa mpango ya kupanua mji wa mkuu Addis Ababa kwenda eneo la Oromia ungesababisha kuhama kwa wakulima wa Oromo. Hata hivyo serilia ilitupilia mbalia mpango huo ambao ungeanza mwezi Januari

mashabiki wa urusi kufukuzwa ufaransa

MTEULE THE BEST     Kiongozi wa chama cha mashabiki wa kandanda nchini Urusi, anatimuliwa kutoka nchini Ufaransa kufuatia ghasia zilizotokea wakati wa mechi za kuwania kombe la taifa bingwa barani Ulaya, kati ya Urusi na Uingereza mjini Marseille. Alexander Shprygin ni mmoja wa mashabiki 20 wa Urusi wanaotimuliwa kutoka Ufaransa. Walikamatwa siku ya Jumanne wakiwa safarini kutoka Marseille kwenda Lille kudhudhuria mechi kati ya Urusi na Slovakia   Ghasia za mashabiki Kukamatwa kwao kuliikasirisha urusi iliyomuita balozi wa Ufaransa humo kupinga. Chama hicho cha mashabiki kinachoongozwa na Shprygin kinaungwa mkono na serikali ya Urusi. Mashabikia wa uingereza na Urusi walipamabana kabala ya na baada ya timu hizo kucheza siku ya Jumamosi. Polisi wa ...

Ratiba mechi za Ligi Kuu ya Uongereza msimu wa 2016/17

MTEULE THE BEST    NATAZAMIA MAKUBWA MSIMU HUU KWA MASHABIKI WENZANGU WA MANCHESTER UNITED KWA JOSE MTEULE G KAHANGILE Ratiba mechi za Ligi Kuu ya Uongereza msimu wa 2016/17 Jumamosi 13 Agosti 2016 LIGI YA PREMIA Arsenal v Liverpool 15:00 Bournemouth v Man Utd 15:00 Burnley v Swansea 15:00 Chelsea v West Ham 15:00 Crystal Palace v West Brom 15:00 Everton v Tottenham 15:00 Hull v Leicester 15:00 Man City v Sunderland 15:00 Middlesbrough v Stoke 15:00 Southampton v Watford 15:00 15:00 Jumamosi 20 Agosti 2016 LIGI YA PREMIA Leicester v Arsenal 15:00 Liverpool v Burnley 15:00 Man Utd v Southampton 15:00 Stoke v Man City 15:00 Sunderland v Middlesbrough 15:00 Swansea v Hull 15:00 Tottenham v Crystal Palace 15:00 Watford v Chelsea 15:00 West Brom v Everton 15:00 West Ham v Bourn...

Ufisadi Bodi mikopo ya wanafunzi Tanzania

MTEULE THE BEST Ripoti ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa na Waziri Elimu wa Tanzania Profesa Joyce Ndalichako imeibua ufisadi katika bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini Tanzania. Ufisadi huo ni pamoja na bodi kutoa mikopo isiyojulikana kwa wanafunzi zaidi 2000 wa kiasi cha shilingi bilion 14 za Tanzania sawa na dola milioni 7 za marekani. Kamati hiyo iliundwa baada ya kusimamishwa kwa watendaji wakuu wa bodi hiyo. Aidha bodi hiyo imegundua upotevu wa Zaidi ya dola Milioni 1.3 zilizolipwa kwa wanafunzi wa vyuo kadhaa ambazo hazitambuliwi na vyuo hivyo huku fedha hizo zikiwa hazijarudishwa. Waziri huyo amesema kuwa baada ya kuyabaini mambo hayo,serikali serikali imechukua hatua za kutoa wiki mbili kwa bodi ya mikopo kuwachukulia hatua mara moja wote wanaohusika ikiwemo watumishi waliosimamishwa. February mwaka huu waziri huyo aliwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wakuu wa bodi hiyo baada ya kubaini udhaifu katika utekelezaji wa majukumu yake ambapo pia ameagiz...

Casillas:nasubili Buffon astafu

MTEULE THE BEST     Casillas kasema anasubiri kwanza Buffon astaafu kisha naye atafuatia KIPA na nahodha wa Hispania Iker Casillas amesema hatastaafu mchezo wa soka mpaka pale kipa na nahodha wa timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Buffon atakaposema imetosha yaani amestaafu. Akiongea na Jarida la Michezo la Italia la La Gazzetta Dello Sport, kutokea nchini Ufaransa   alikokwenda kuitumikia Hispania katika michuano ya Ulaya (Euro) Casillas,35, amesema haoni sababu ya kustaafu kwasasa wakati wachezaji wenye umri mkubwa kuliko yeye kama swahiba wake,Gianluigi Buffon bado wanatamba viwanjani. Amesema "Kuhusu kustaafu! Nadhani Buffon atakapostaafu,nitastaafu pia. Amesaini mkataba mpya hivi karibuni na hilo litanifanya niwe na furaha kwa sababu nina imani na mimi nitasaini pia. "Muda wetu wa kustaafu utakapofika,tutaandaa mchezo kati ya marafiki zangu na marafiki zake kuhitimisha zama zetu" Kauli hiyo ya Casillas imekuja baada y...