Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mashambulizi dhidi ya Syria hayakuwa halali-Ripoti ya Bunge la Ujerumani

Ripoti ya wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani imesema mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Syria mapema mwezi Aprili yalikiuka sheria ya kimataifa. Ripoti ya wataalamu wa sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani, imesema mashambulizi yaliyofanywa na nchi tatu za Magharibi hayakuwa halali kisheria. Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliishambulia Syria kwa makombora tarehe 14 Aprili, kwa madai kwamba zilikuwa zikiiadhibu serikali ya Rais Bashar al-Assad, ziliyemshutumu kutumia gesi ya sumu kuwashambulia raia katika mji wa Douma. ''Matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya nchi huru, kama hatua dhidi ya ukiukaji wa sheria na kanuni za kimataifa unaodaiwa kufanywa na nchi inayoshambuliwa, ni uvunjaji a sheria ya kimataifa inayozuia matumizi ya ghasia,'' imesema ripoti hiyo ya wataalamu wa kisheria wa Bunge la Ujerumani, Bundestag. Ripoti hiyo iliombwa na chama cha mrengo wa kushoto (Die-Linke) cha Uj...

Malkia Elizabeth II wa Uingereza atimiza miaka 92

Wizi wa almasi: Mugabe atakiwa kutoa ushahidi

Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi. Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi. Bwana Mugabe alizishutumu kampuni za kigeni za kuchimba madini kwa ''kuiba'' na ''kusafirisha'' katika mahojiano na runinga ya taifa 2016. ''Kampuni hizo zimetuibia utajiri wetu'' , alisema. Akiongzea kuwa wizara ya fedha ilipokea $15bn pekee. Haijulikani iwapo raia huyo mwenye umri wa miaka 94 atakubali kufika mbele ya kamati hiyo ya bunge. Alilazimishwa kujiuzulu mwezi Disemba iliopita kufuatia mapinduzi ya kijeshi na bado anahudumiwa na serikali kama rais wa zamani

Bashar al-Assad arudisha tuzo aliyopewa na Ufaransa

Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascus. Syria imerejesha kwa Ufaransa tuzo ya Légion d'honneur aliyopewa rais Bashar al-Assad, ikisema kuwa haiwezi kuchukua tuzo kwa taifa ambalo limekuwa 'mtumwa' wa Marekani. Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Ufaransa kusema kuwa adhabu ya kuikataa tuzo hiyo inakaribia. Ufaransa hivi majuzi ilijiunga na Ufaransa na Uingreza katika kuishambulia Syria kufuatia madai ya kutumia silaha za kinyuklia dhidi ya raia wake. Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascus. Rais Assad alipewa tuzo hiyo ya hadhi ya juu 2001 baada ya kuchukua mamlaka kufautia kifo cha babake. ''Wizara ya maswala ya kigeni imerudisha kwa Jamhuri ya Ufaransa tuzo ya Légion d'honneuri iliopewa rais Assad'', wizara ya kigeni nchini Syria ilisema katika taarifa. ''Sio heshima kwa rais Assad kuvaa tuzo iliotolewa na taifa la utumwa na mshiriki wa taifa la Marekani li...

Korea Kaskazini yasitisha majario ya nyuklia na makombora

Korea Kaskazini imetangaza kusitisha mara moja majaribio yote ya silaha za nyuklia na makombora ili kujikita katika kusaka maendeleo ya kiuchimi na amani kwenye rasi ya Korea.Imetangaza pia kufunga kituo cha majaribio. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema nchi yake haihitaji tena kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu kwa sababu imekamilisha lengo lake la kutengeneza silaha za nyuklia, limeripoti shirika la habari la nchi hiyo KCNA. Korea Kaskazini imesema ili kuunda mazingira ya kimataifa yenye kufaa kwa uchumi wake, itawezesha mawasiliano ya karibu na mjadala pamoja na mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Korea Kaskazini kuzungumzia moja kwa moja mpango wake wa silaha za nyuklia, na imekuja siku kadhaa kabla ya mkutano wa kilele unaoandaliwa kati ya Kim na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in wiki ijayo, na mkutano na rais wa Marekani Donald Trump mwishoni mwa mwezi Mei au mwanzoni mwa Juni. "Uwanja wa kaskazini wa majaribio...

Tanzania yafafanua madai ya upotevu wa trilioni 1.5

Baada ya juma zima la kuwepo kwa hofu ya kutoweka kiasi cha shilingi trilioni 1.5 za Kitanzania serikalini, hatimaye leo serikali ya Rais John Magufuli imetoa ufafanuzi bungeni juu ya wapi kilipo kiasi hicho cha fedha. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli. Baada ya juma zima la kuwepo kwa hofu ya kutoweka kiasi cha shilingi trilioni 1.5 za Kitanzania katika mazingira ya kutatanisha katika makadirio ya bajeti ya serikali ya Tanzania, hatimaye leo serikali ya Rais John Magufuli imetoa ufafanuzi bungeni juu ya wapi kilipo kiasi hicho cha fedha. Ufafanuzi huu unatolewa baada ya kuwepo kwa kile kilichoonekana kama ukosoaji wa wazi na wasiwasi juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma na yasiozingatia sheria kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani na hata wananchi wa kawaida kwa takribani juma zima. Akitoa mchanganuo wake, Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji amesema kiasi cha shilingi bilioni 697 kilitumika kwa matumizi ya dhamana...

Kuna mipaka kati ya uhuru wa kujieleza na Maadili?

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha GOOGLE Image caption Watumiaji wa mitandao wamekuwa wakilaumiwa kukiuka maadili Mitandao ya kijamii ni majukwaa ya kutoa maoni. Jamii imekuwa ikitumia majukwaa hayo kujieleza kwa kutumia sanaa, kutoa hotuba, kutoa mawazo au maoni, kwa njia ya maandishi, picha au michoro. Mitandao kama Facebook, Tweeter, Instagram, Snapchat, Jamii forum, Whatsapp na mingine mingi imetumika kwa muda mrefu kutimiza azma hiyo. Hata hivyo watumiaji wamekuwa wakikosolewa kwa kiasi kikubwa kuhusu namna wanavyoitumia mitandao hiyo. Ukuwaji wa matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa watanzania hasa vijana umeifanya serikali ya Tanzania kuweka  Sheria ya Kukabiliana na uhalifu Mitandaoni  mwaka 2015 ambayo tangu wakati huo imekuwa ikikosolewa kwa kuwaandama watumiaji wa kawaida wa mitandao hiyo. Ukiukaji wa maadili Wiki moja baada ya kampeni ya #ifikiewazazi kusambaa mitandaoni nchini Kenya, mamlaka ilianza kuwatafuta vijana waliokuwa wamepiga picha...