Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Tanzania yaitaka Mwananchi kuomba radhi kwa taarifa kuhusu deni la taifa

Rais Magufuli majuzi aliwataka wananchi kuwapuuza wanaodai serikali inakopa sana Serikali ya Tanzania imesema deni la jumla la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 3 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Desemba hadi Machi mwaka huu. Serikali hiyo imepuuzilia mbali taarifa zilizochapishwa na gazeti moja nchini humo zilizodai kwamba deni la taifa hilo la Afrika Mashariki liliongezeka Sh trilioni 12 katika kipindi hicho. Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amelitaka gazeti la mwananchi "kuomba radhi kwa umma kwa siku mbili mfululizo kuanzia kesho Jumapili" kupitia ukurasa wa mbele wa gazeti hilo na kwenye mitandao ya kijamii. Dkt Abbas amesema baada ya gazeti hilo kusisitiza "kuwa hawana nia mbaya, serikali imezingatia utetezi huo na inawapa nafasi ya kujirekebisha zaidi". Taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya Benki Kuu ya Tanzania inasema katika kipindi hicho, deni la serikali liliongezeka ...

Kwa Picha: Harusi ya kifalme ya Prince Harry na Meghan Markle

Mkusanyiko  wa picha  za kuvutia zaidi  kutoka kwa harusi ya kifalme kati ya  Mwanamfalme Harry na Meghan Markle. Umati ulishangilia Mwanamfalme Harry, ambaye sasa atakuwa Mtawala wa Sussex, na mkewe Meghan, Mke wa Mtawala wa Sussex, walipopitia kwenye barabara za mji wakiwa kwenye kigari cha kuvutwa kwa farasi Inakadiriwa kwamba 100,000 walijitokeza barabara za Windsor Umati wa watu ulikusanyika kando ya barabara kutazama msafara wa harusi ukipita Meghan na Mwanamfalme Harry wakiondoka kanisa la St George  Ragland, mamake bi harusi, Charles Mtawala wa Cornwall (babake Harry) na mkewe Camilla wakiondoka kanisani  Wakiondoka kanisani Waliokuwemo walishangilia wawili hao walipokuwa wanapigana busu Wawili hao wakipigana busu Wawili hao wakiondoka kanisani baada ya kufunganishwa katika ndoa Harry na Meghan sasa watakuwa Mtawala na Mke wa Mtawala wa Sussex Malkia na mumewe, Mwanamfalme Phillip walihudhuria sherehe hiyo Mwanamfalme Harry akimfunua Megh...

Putin afanya mazungumzo na Merkel mjini Sochi

Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema leo kuwa nchi za Ulaya zinapaswa kusaidia kuijenga Syria ikiwa zinataka wakimbizi warudi nchini mwao. Akizungumza pamoja na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel katika mji wa kusini mwa Urusi wa Sochi, Putin amesema ujenzi wa Syria haupaswi kuingizwa siasa. Urusi inapinga msimamo wa Umoja wa Ulaya kuwa nchi za Magharibi zitazingatia tu msaada wa kiutu lakini hazitatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Syria kama Rais Bashar al Assad atakataa kugawana madaraka na upinzani. Merkel amemtaka Putin kutumia ushawishi wake kwa Assad kumfanya aibatilishe sheria ambayo itawapokonya Wasyria mali zao kama watashindwa kuzidai mara moja. Putin alikutana na Assad jana mjini Sochi na kumhimiza achukue hatua za kutafuta suluhisho la kisiasa

Visa vya Ebola vyaongezeka Congo

Wizara ya afya ya nchini Congo imesema idadi ya visa vya homa ya Ebola vilivyothibitishwa nchini humo vimeongezeka kutoka watu watatu na kufikia watu 14. Wizara hiyo imesema mtu mmoja pekee ndiye aliyethibitishwa kufariki dunia ingawa kuna madai kwamba watu 25 wamefariki. Maafisa wa afya wako mbioni kuidhibiti homa hiyo inayosambazwa na virusi na ambayo kwa sasa imethibitishwa katika mji wa Mbandaka wenye watu zaidi ya milioni moja. Mbandaka ni mji ambao hauko mbali na Mji Mkuu Kinshasa na uko katika Mto Congo ambao ni eneo lenye shughuli nyingi za usafiri. Shirika la Afya Duniani, WHO limefanya kikao cha dharura leo na kutangaza kwamba tahadhari ya kuenea kwa maradhi hayo imeongezeka kutoka "juu" na sasa imefikia kuwa "juu mno". Shirika hilo linasema kuwa tahadhari katika nchi zilizoko katika kanda hiyo imeongezeka pia kutoka kiwango cha "wastani" na sasa imefikia kiwango cha "juu", ingawa tahadhari ya maradhi hayo kuenea dunia nzi...

Je Ukraine itaenedelea kupokea gesi kutoka Urusi?

Rais wa Urusi Vladimir Putin amemwambia kansela Angela Merkel kwamba gesi ya asili ya Urusi inaweza kupelekwa kwenye nchi jirani ya Ukraine iwapo yatakuwepo manufaa ya kiuchumi kwa Urusi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Urusi Vladimir Putin kwenye mazungumzo yao wamejadiliana kuhusu mgogoro wa nchini Ukraine, wakati ambapo Urusi inaongeza ukubwa wa bomba lake la gesi ya asili kwenda moja kwa moja hadi nchini Ujerumani, bila kupitia Ukraine. Rais Putin na Waziri wake Mkuu Dmitry Medvedev walimkaribisha Kansela Merkel katika makao ya rais ya majira ya kiangazi yaliyopo katika jiji la kusini mwa Urusi la Sochi, kansela Merkel ndiye aliyeongoza vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi wakati nchi hiyo ilipolitwaa jimbo la Crimea miaka minne iliyopita. Lakini katika miezi ya hivi karibuni, Ujerumani ilitoa idhini yake kwa Urusi kuweza kutanua bomba lake la gesi la Nord Stream, ambalo litasafirisha gesi ya asili hadi nchini Ujerumani licha ya Ukraine kuupinga mra...

Switzeland yaahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania

Switzeland imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kusaidia sekta mbalimbali za Maendeleo hususan katika suala la afya, kuongeza ajira na kukuza ujuzi . Hayo yamebainishwa wakati wa Mkutano uliofanyika Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango na Balozi wa Switzerland nchini, Florence Tinguely Mattli, uliojaili uhusiano kati ya nchi hizo mbili na namna ya kuboresha ushirikiano. Katika Mkutano huo, Waziri Mpango amemuomba Balozi huyo kuangalia uwezekano wa kuwapa mafunzo madaktari Bingwa nchini ili kukidhi uhitaji uliopo hususan katika Jiji la Dodoma ambalo ndiyo makao Makuu ya Nchi na  idadi ya wakazi wake inaongezeka. Pia amemuomba kufadhili mafunzo kwa watumishi wa umma ili kuwajengea uwezo katika kada mbalimbali lengo likiwa ni  kuongeza ufanisi kazini. Aidha kuhusu suala la uboreshaji miundombinu ya Jiji la Dodoma, Waziri Mpango aliiomba Switzerland kuangalia uwezekano wa kufadhili miradi ya maendeleo katika sekta ya maji na m...

Rais Magufuli kuikabidhi Simba kombe la ubingwa wa VPL

mteulethebest Rais wa Tanzani, John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara (VPL) kati ya mabingwa wapya Simba SC na Kagera Sugar utakaochezwa Jumamosi Mei 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema wamemuandikia barua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kumuomba Rais Magufuli awe mgeni Rasmi kwenye mchezo huo. Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli endapo atakubali wito huo, atapata nafasi ya kuwakabidhi Simba Kombe la VPL, sanjari na kuikabidhi  Timu ya Taifa ya soka ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys  kombe la CECAFA kwa vijana walilotwaa siku za karibuni nchini Burundi. Amesema mchezo kati ya Simba na Kagera Sugar utaanza saa 8:00 mchana badala ya Jumapili saa 10:00 jioni ili kutoa fursa kwa sherehe hizo kufanyika kikamilifu.