Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Watu 20 wafariki dunia katika ajali ya barabarani Mbeya, Tanzania

Takriban watu 20 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha zaidi ya magari matatu mkoani Mbeya, kanda ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Ajali hiyo ilitokea katika mteremko wa Iwambi mkoani Mbeya. Hii ni ajali ya tatu kutokea Mbeya katika kipindi kifupi ambapo katika ajali hizo idadi ya Watanzania waliopoteza maisha imefikia 40. Mnamo 14 Juni, watu 13 wakiwemo vijana 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), askari 1 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na dereva walipoteza maisha, na jumla ya watu 25 wakajeruhiwa, majira ya mchana baada ya ajali kutoka katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya. Aprili, watu wanane waliokuwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Noah walifariki dunia papo hapo baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi katika eneo la Igodima. Gari hilo lililokuwa likitokea Chunya kwenda Mbeya mjini, lilikuwa na abiria tisa waliokuwa wakienda katika msiba wa ndugu yao. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoan...

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 02.07.2018

Juan Quintero Wolves wamejaribu kumasaini kiungo wa kati wa Colombia Juan Quintero ambaye ameonyesha mchezo mzuri kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid na Tottenham kwa mchezaji huyo wa miaka 25. (Mirror) Chelsea wanamteua meneja mpya Maurizio Sari leo Jumatatu na mchezaji ambaye atamsaini kwanza ni kiungo wa kati wa Urusi Aleksandr Golovin, 22, ambaye atagharimu pauni milioni 27 kutoka CSKA Moscow. (Sun) Alassane Plea West Ham na Fulham wanamenyana kwa pauni milioni 25 kumsaini mshambuliaji wa Nice Mfaransa Alassane Plea, 25. (Sun) Newcasle pia nao wanammezea mate mshambuliaji wa zamani wa Lyon Plea, ambaye alifunga mabao 21 kwenye mashindano ya msimu uliopita. (Shields Gazette) Andros Townsend Newcasle wanatathmini ofa kwa wing'a wa Crystal Palace muingereza Andros Townsend, 26, lakini ikiwa tu wataamua kumuuza wing'a msikochi Matt Ritchie, 28, kwenda Stoke City. (Telegraph) Juventus wamekataa ofa ya Lazio...

Mabadiliko baraza la mawaziri Tanzania: Magufuli amfuta kazi Mwigulu Nchemba, Zitto Kabwe na Pole Pole walumbana

Mwigulu Nchemba Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri chini ya kipindi cha mwaka mmoja Aliyeathirika na mabadiliko ya Rais Magufuli siku ya Jumapili ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Mwigulu Nchemba alipata umaarufu kwa juhudi zake za kuzuia maandamano dhidi ya Rais Magufuli. Alinukuliwa akitishia kuwalemaza waandamanaji na ''kuwakamata hata watakaoandamana wakiwa nyumbani". Licha ya hapo awali kuhamishwa kutoka wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi, hadi wadhfa wake wa mwisho, Nchemba ameondolewa baada ya kuhudumu kwa miaka miwili katika baraza la Rais Magufuli. Mbunge huyo wa Iramba aliyechukua nafasi ya aliyekuwa waziri Charles Kitwanga, sasa atampisha mbunge mwenzake kutoka Jimbo la Mwibara, Kangi Alphaxard Lugola kujaza pengo hilo. Ruka ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe Lugola amepandishwa ...

Chimbuko la mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylian Mbappe

Lionel Messi na Kylian Mbappe walipokumbatiana kipenga cha mwisho baada ya mechi yao, ilitoa taswira ya kupokezana kwa kijiti cha ubora kutoka nyota hadi mwingine. Kila mmoja aliyehudhuria mchuano huo wa kukata na shoka, aliaga uga wa Kazan Jumamosi akihisi kushuhudia mechi spesheli itakayosalia akilini kwa miaka. Kwa kifupi, ni mchezaji mmoja alichukua sifa zote siku hiyo Mbappe ana umri wa miaka 19 tu lakini amefunga mabao mawili muhimu na kuchomoka kwa kasi kutoka kitovu cha uwanja na kupelekea penalti iliyoipa Ufaransa bao la ufunguzi wakati ilipoichabanga Argentina 4-3. Ushindi huo umewafikisha vijana wenye vipawa wa Didier Deschamp robo fainali. Ni maonyesho yaliyofichua uwezo kamili wa Ufaransa kufika fainali Urusi 2018 na kuondoka na Kombe la Dunia kwa mara ya pili. Mbappe - Mshambulizi mwenye ukwasi wa talanta Mbappe hakuzaliwa Ufaransa ilipotwaa Kombe la Dunia ikiwa nyumbani 1998. Cha kustajaabisha, Mbappe alifufua kumbukumbu za mchezo wa Michael Owen na usumbufu...

Viongozi wa mataifa ya Afrika wakutana Mauritania

Viongozi wa  Afrika wanakutana Mauritania Jumapili(01.07.2018)katika mkutano wa siku mbili utakaolenga biashara huria, upatikanaji wa fedha, mapambano dhidi ya rushwa pamoja na mizozo mingi  ya kiusalama barani humo. Zaidi  ya  viongozi  wa  serikali  na  taifa  40 wanatarajiwa  kuwasili  katika  mji  mkuu  wa Mauritania  , Nouakchott, wakiungana  siku  ya  Jumatatu na  rais  wa  Ufaransa  Emmanuel Macron , ambaye  anatarajiwa  kusukuma juhudi  za  kiusalama  katika  eneo  la  Afrika kaskazini. Kiongozi  wa  Rwanda  Paul Kagame, ambaye anashikilia  urais wa  kupokezana  wa  Umoja wa  Afrika  ( AU )wenye  wanachama  55, atatoa  rai  kuhimiza  biashara  huru. Paul Kagame (kulia) akisalimiana na ...

Redoine Faid: Jambazi sugu aliyetoroka jela kwa kutumia helikopta Ufaransa

Jambazi sugu ametoroka jela kwa kutumia ndege aina ya helikopta katika jela moja mjini Paris , mamlaka ya Paris imesema. Redoine Faid alisaidiwa na watu kadhaa waliojihami ambao walitengeneza mwanya katika lango la jela hiyo huku helikopta hiyo ikitua katika uwanja karibu na jela hiyo. Ndege hiyo ilipaa hadi eneo la Gonessa lililopo karibu na jela hiyo ambapo ilipatikana na maafisa wa polisi. Faid 46, amekuwa akihudumia kifungo cha miaka 25 kwa jaribio la wizi wa mabavu lililotibuka ambapo afisa mmoja wa polisi aliuawa. Hii ni mara yake ya pili kutoroka jela: Mwaka 2013 alitoroka jela baada ya kuwatumia walinzi wanne kama ngao huku akilipua milango kadhaa kwa kutumia kilipuzi. Alifanikiwa kutoroka chini ya nusu saa baada ya kuwasili katika jela hiyo iliopo kaskazini mwa Ufaransa. Mwaka 2009 Faid aliandika kitabu kuhusu uzoefu wake katika mitaa ya Paris iliojaa uhalifu na kuwa mtu aliyekukuwa akivunja sheria mara kwa mara. Alidai kuwacha uhalifu lakini mwaka mmoja baad...

Biashara ya shirika la ndege la Air Tanzania yaimarika

Biashara ya shirika la ndege la AIR Tanzania Company Limited (ATCL) imepanda thamani kwa kipindi cha miaka miwili licha ya kuwa na abiria wachache waliotumia ndege zake kusafiria Mkurugenzi wa biashara wa ATCL Patrick Ndekana aliambia gazeti la  D aily News  kwamba biashara za shirika hilo la serikali iliongezeka kutoka asilimia 2.5 mwaka 2016 hadi asilimia 42.6 mwisho wa mwaka jana huku ikiwa na ndege mbili pekee zinazofanya kazi. Amesema kuwa wana matumaini kwamba biashara hiyo itaimarika zaidi baada ya kununuliwa kwa ndege mpya. ''Mwaka huu biashara yetu itaongezeka hususan baada ya kuwasili kwa ndege ya tatu kubwa aina ya Bombadier Q-400s na baadaye kuwasili kwa Bombadier nyengine mbili za Cs 300s ambazo zitakuwa na viti vingi'', alisema. Kwa sasa shirika hilo linamiliki ndege tatu aina ya Q-400 katika maeneo 10 tofauti nchini, mbali na kuelekea Comoro. Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka jana, shirika hilo limekuwa likisafirisha abi...