MTEULE THE BEST

Ndoa siku hizi zimekua kama fashion yaan watu wanazikimbilia kwa kukurupuka kisa michango ya harusi, kuiga n. k ila ukweli unabaki hakika yafuatayo yanawaponza mno wanandoa wengi nchini:
1: Wahusika kuingia katika ndoa pasipo kuwa na ufahamu juu ya ndoa. Wengi huingia kwa kufuata mazoea tu kwamba, umri fulani ukifika basi huwa ni wakati wa kuoa au kuolewa. Wengine huingia kwenye ndoa ili kujionyesha kwa jamii tu kwa kuwa na sherehe ya harusi ya kifahari. Watu hao utawagundua mapema tu, maana husisitiza sana juu ya sherehe za kifahari maana hawana future na wewe, hata kukopa kwa ajili ya sherehe wako tayari.
2: Kukosa mifano mizuri ya namna ya kuendesha ndoa imara yenye furaha katika jamii, hususani kutoka kwa wazazi wao. Wazazi wenyewe wamekuwa si mfano mzuri juu ya ndoa bora. Wazazi kuwa ndoa zenye migogoro isiyoisha, imekuwa mafundisho mabaya kwa watoto wao. Kama baba hupiga mke wake, ni wazi kuwa mtoto wake pia ataishi kwa kupiga mkewe maana hivyo ndivyo alivyoaminishwa na wazazi wake.

4: Utandawazi. Hii nayo ni changamoto kubwa kabisa kwenye ustawi wa ndoa kwa mfano, 50/50 inayopigiwa chapuo na wanasiasa wanawake na wanaharakati na kumbe si hitaji la mwanamke halisi (mwanamke wa kawaida). Watu hawa wanaopigia debe hii mambo ya 50/50 wana interest zao. Na hivyo, wamekuwa wakiwachanganya wanawake walioko kwenye ndoa.
5: Kuingia kwenye ndoa kwa lengo la kwenda kutumikiwa na siyo kutumika. Ni tatizo kubwa mno kuoa au kuolewa ukiwa na mtazamo kuwa huyo mwenzi wako ndiyo anakuwa mtumwa wako.
6: Kumlazimisha mwenzi wako awe kama unavyofikiria huku ukisahau kuwa kila mtu ameumbwa kwa kusudi fulani maalumu.
7: Kukosa roho ya toba na kusameheana. Ni tatizo kubwa kwamba kizazi kimekuwa kikaidi. Kila mmoja hujihesabia haki, na hivyo kukosa mwenye kuomba msamaha kila mgogoro utokeapo.
8: Mila na desturi nazo ni tatizo hasa wanandoa wanapokuwa wametoka katika malezi tofauti au mila tofauti na bila wao kuwa na uelewa kuwa wanatakiwa kuachilia yale waliyojifunza nyuma ili kuweza kuendandana na wenzi wao.
9: Kukosa commitment juu ya kuwa na ndoa imara, ndoa yenye ushuhuda, ndoa inayomtukuza Mungu. Wengi huishi maisha ya unafiki, wakiwa ndani hawana maelewano hata vitanda wameachanisha, lakini wakiwa nje utadhani hawana mgogoro. Bwana Yesu asifiwe nyingi sana!!

11: Ushauri mbaya toka kwa marafiki na jamii kwa ujumla. Kwa mfano, mwanaume kushauriwa kuwa haifai kumuomba msamaha mwanamke hata kama amekosea, eti kwa madai kuwa akifanya hivyo mwanamke atamuona dhaifu! Mwanamke kushauriwa kuwa mwanaume akikukosea dawa yake ni kumnyima unyumba.
Lakini naomba nikuambie kuwa, mwanaume halisi huomba msamaha mapema sana mara tu agunduapo amemkosea mkewe, huyo ndiyo mwanaume halisi. Mwanamke kamwe, kamwe hapa duniani usithubutu kutumia unyumba kama fimbo kwa mumeo, kamwe!
Nakutakia kila la kheri iwapo upo katika ndoa au unatarajia kuingia katika ndoa, Mungu akubariki na kukuongoza. Kumbuka ni bora kukosea kujenga nyumba kuliko kukosea kuoa au kuolewa na mtu asiye sahihi UTAJUTIA MNO
Kama umeipenda SHARE na marafiki
Maoni