MTEULE THE BEST
Mkufunzi Jose Mourinho amesema kuwa
yuko tayari kuchukua jukumu la kuifunza Manchester United, lakini
akaonekana pia kumkejeli meneja wa Arsenal Arsene Wenger.
Amesema ''niko mahala nitakapo''.Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 aliongezea: ''Nadhani ni kazi ambayo kila mtu anahitaji na sio wengi ambao huipata na mimi nimeipata''.
Alipoulizwa iwapo ana chochote cha kujionyesha baada ya kufutwa kazi akiwa Chelsea, alijibu, akionekana kumrejelea Wenger: ''Kuna mameneja ambao hawajashinda mataji kwa kipindi cha miaka 10 iliopita. Wengine bado kabisa. Mara yangu ya mwisho kushinda taji ni mwaka uliopita''.

Mourinho anasema kuwa anachukizwa kuona kwamba United haitashiriki katika mechi za kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao lakini akasisiiza kuwa yuko Old Trafford kushinda mataji.
Arsene Wenger
Nataka kushinda mechi,nataka kucheza vizuri sitaki kufungwa magoli.nataka mashabiki kutuunga mkono.
Maoni