Tetesi za usajili ulaya 2016
MTEULE THE BEST
Mshambuliaji wa England na Tottenham,
Harry Kane atasaini mkataba mpya kusalia White Hart Lane wenye thamani
ya pauni milioni 5 kwa mwaka wiki hii (Independent), Jose Mourinho ana
uhakika wa kumshawishi kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, kurejea
tena Manchester United miaka minne baada ya kuondoka na kwenda Juventus
(Daily Mail), Manchester United wapo tayari 'kuvunja benki' ili
kumsajili Pogba, huku dau likidhaniwa kufika hadi pauni milioni 100
(Telegraph).
Kiungo wa Paris St-Germain, Blaise Matuidi, 29,
amepewa ruhusa ya kuondoka katika kambi ya Euro 2016 ya Ufaransa na
kwenda England kwa ajili ya mazungumzo ya kuhamia Manchester United
(Goal), Manchester United na Liverpool wote wanataka kumsajili kiungo wa
Porto Ruben Neves, 19 (Sun), Manchester City wanakaribia kukamilisha
usajili mwingine unaodhaniwa kuwa wa pauni milioni 40 kumchukua winga wa
Schalke, Leroy Sane, 20 (Manchester Evening News), Tottenham hatimaye
wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa AZ Alkmaar, Vincent
Janssen, 21, wiki hii na pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Roma,
Antonio Sababria, 20 na Lucas Alario, 20 kutoka River Plate (Daily
Mirror).
Arsenal wako tayari kumpa Alvaro Morata, 23,
mshahara wa pauni 144,000 kwa wiki kumshawishi kuhamia Emirates (Don
Balon), Crystal Palace wameongeza dau lao kufikia pauni milioni 31.5
kumtaka mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke, 25, baada ya dau la
pauni milioni 25 kukataliwa (Sun), Crystal Palace wanakamilisha
uhamisho wa beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Evening Standard),
Chelsea wanafikiria kutoa pauni milioni 12 kumchukua mshambuliaji wa
Southampton Graziano Pelle, 30, iwapo watashindwa kumpata Morata kutoka
Real Madrid (Evening Standard).mbazo Robin van Persie, 32, ameruhusiwa kwenda na klabu yake ya Fernabahce (Daily Mail), mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Charles N'Zogbia, 29, anajaribu kufufua mpira wake kwa kufanya mazoezi na Sunderland (Birmingham Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Maoni